27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

TIMU 20 KUSHIRIKI CHEMCHEM CUP

                                                                  |Janeth Mushi, Babati



Jumla ya timu 20 zinatarajiwa kushiriki Ligi ya Chemchem Cup,wilayani Babati, mkoani Manyara ambapo mshindi ataondoka na zawadi zenye thamani ya Sh milioni 4.5.

Kwa mujibu wa Mratibu wa ligi hiyo ambayo hufanyika kila mwaka, Charles Goodlucky lengo la mashindano hayo yatakayofanyika katika Uwanja wa Mdori, yana lengo la kupiga vita ujangili na kuhamasisha jamii juu ya masuala ya uhifadhi wa mazingira.

Amesema mashindano hayo yatafunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti Agosti 19 mwaka huu.

“Katika mashindano ya mwaka huu, timu hizo tumezitaka zithibitishe kushiriki ligi hiyo na kushiriki kwenye kikao kwa ajili ya kupanga ratiba ya ligi husika.

“Mwaka huu bingwa wa soka atapewa zawadi ya fedha taslimu Sh milioni 1.7 na kombe, mshindi wa pili milioni 1.1, mshindi wa tatu Sh 600,000 na mshindi wa nne Sh 300,000, lakini pia kutakuwa na zawadi kwa kocha bora, timu bora na mchezaji bora,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, amesema katika michuano hiyo pia kutakuwa na michezo ya wanawake ambapo bingwa atazawadiwa Sh 400,000, ngoma za kitamaduni na michezo mingine.

Awali Meneja wa Taasisi ya Chemchem Foundation, Recardo Tossi, alisema ligi hiyo imekuwa ikishirikisha zaidi ya wanamichezo 400 kila mwaka.

“Ligi hii hukutanisha wanamichezo wengi na lengo ni kutaka jamii inayozunguka kijiji cha Mdori na Tarafa nzima ya Mbugwe katika wilaya yetu ya Babati kuwa wahifadhi wazuri na kupinga ujangili na kuhifadhi mazingira,” amesema.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles