27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

TIKETI 244 ZANUNULIWA UJIO DREAMLINER MWANZA

Na PETER FABIAN-MWANZA

WAKATI ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner ikitarajiwa kutua jijini Mwanza kesho, Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Ofisi ya Kanda ya Ziwa, limesema kwamba, hadi kufikia juzi tiketi 244 zimenunuliwa kwa safari ya asubuhi kurudi jijini Dar es Salaam.

Taarifa hiyo ilitolewa juzi na Meneja wa ATCL Kanda ya Ziwa, Theonestina Ndyetabula, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kuipokea ndege hiyo.

“Niwaombe wadau na wananchi kujitokeza kwa wingi kuja kushiriki mapokezi ya ujio wa ndege mpya ya Boeing 787-8 Dreamliner, yenye daraja la biashara (viti 22) na kawaida (Economy) viti 240, hivyo jumla ni abiria 262 …nawahakikishia wananchi na abiria wanaotumia ndege za shirika letu kuwa watapata huduma bora na gharama rafiki wakati wote, pia waepuke baadhi ya mawakala wasio waaminifu wanaolihujumu wakijinadi kuwa ndege zetu zina gharama sawa na makampuni mengine,” alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, akizungumzia ujio wa ndege hiyo, alisema kwamba, taarifa njema ni abiria 244 wanaotumia Uwanja wa Ndege wa Mwanza wataruka na ndege ya Dreamliner baada ya kutua jijini Mwanza kwa mara ya kwanza ikitokea Dar es Salaam kupitia Kilimanjaro Julai 29, mwaka huu, asubuhi, huku tiketi 158 zikiwa zimeuzwa kwa abiria wa ndege ya usiku siku hiyo.

Mongella alisema kwamba, wananchi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa watumie fursa hiyo kusafiri na ndege za ATCL ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano, iliyoanza kutekeleza azma yake ya kulirejesha shirika hilo katika ubora wa kuwa na uhakika wa safari zake za ndani na baadhi ya mataifa ya Afrika na Asia.

Mongella alisema katika mapokezi hayo, wamewaalika wakuu wa mikoa ya Mara, Shinyanga, Simiyu, Geita na Kagera, ambao watawaongoza wadau mbalimbali wa wanaotumia usafiri wa anga na wananchi wa jiji la Mwanza kuipokea ndege mpya katika Uwanja wa Mwanza kwa tukio litakalodumu kwa saa moja.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Hongera ujio wa dreamliner 787-8
    Kuwe na miundo mbinu mizuri itakayorahisisha kwa abiria kutoka mikoa walioalkwa kuipokea ya kuwawezesha kufika Mwanza kwa harska hata wakiwa na bidhaha za kusafirisha haraka kwenda au kutoka Dar es salaam.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles