23.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Tigo warahisisha ulipaji wa maegesho jijini Dar es Salaam

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

Kampuni ya Mawasiliano ya Simu za mkononi ya Tigo Tanzania, imezindua huduma mpya ya kulipa bili ya maegesho kupitia Tigo Pesa ijulikanayo kama “LIPIA PARKING” ambayo itawawezesha watumiaji wa mtandao huo kulipia huduma za maegesho ya magari katika kituo cha ununuzi cha Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Tigo, huduma hiyo itarahisisha malipo ya ada za maegesho ndani ya viwanja vya Milimani City kupitia Tigo Pesa huduma ya USSD Push e-parking.

Akizungumza katika uzinduzi huo, uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Jumatano Juni 15, 2022, Kaimu Mkuu wa Ushirika Tigo Pesa, Haidari Chamshama amesema hatua hiyo itawakilisha hatua nyingine muhimu ya kusukuma huduma za malipokidigitali.

“Hatua hii itawakilisha hatua nyingine muhimu ya kusukuma huduma zetu za malipo ya kidijitali kwenye wigo mwingine, wageni wanaotembelea kituo maarufu cha Mlimani City Shopping kila mara wamekuwa wakilalamika kuhusu muda unaowachukua kulipa ada zao za maegesho. Lipia Parking Kwa Tigo Pesa inaingia sokoni ili kutatua msongamano wa maegesho katika majengo hayo.

“Ili kutumia huduma hii, mteja anahitaji kuchanganua kuskani ‘QR code’ ilio chini ya risiti kwa kutumia kamera ya simu janja yake, kisha ubofye kiungo kinachoonekana kwenye skrini, kisha achague alama ya Tigo Pesa.

“Mteja atahitajika kuingiza nambari ya simu ya Tigo. Ujumbe wa kumbukizi utatokea ambao utahitaji mteja kuweka neno la siri la Tigo Pesa, kisha kuthibitisha muamala,” amesema Chamshama.

Kwa upande mwingine, Meneja Mradi kutoka E-Parking, Beatrice Ndikalo amesema kuzinduliwa kwa huduma hiyo mpya ni moja ya hatua kubwa katika sekta ya maegesho.

“Huduma hii mpya ya malipo ya simu ni hatua kubwa kwa ulimwengu mpya wa maegesho ya kisasa kwani inaruhusu wateja wetu kulipia huduma ya maegesho kwa kuchanganua msimbo wa QR kwenye tiketi zao na kufikia jukwaa la malipo mahali popote kwenye kituo na kuwasaidia kuondokana na foleni.

“Hivyo E-Parking pamoja na Tigo pesa, tumefanya suluhisho hili la malipo ya simu ya mkononi kuwa la mafanikio kwa uzoefu bora wa mteja,” amesema Ndikalo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles