31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Tigo na Milembe Insurance waja na huduma ya bima kidigitali kwa vyombo vya usafiri

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

KAMPUNI ya Tigo Tanzania kwa kushirikiana na Kampuni ya Bima ya MIilembe Insurance wamezindua huduma mpya ya bima ya vyombo vya usafiri ijulikanayo kama TIGO MOTOR INSURANCE, itakayowawezesha wateja wa Tigo Pesa kukatia vyombo vyao vya Usafiri Bima na kukamilisha taratibu zote muhimu Kidigitali kwa kutumia simu zao za mkononi popote pale watakapokua kupitia Tigo Pesa.

Kwa mujibu wa Tigo, Bima hiyo itahusisha aina mbalimbali za magari kama vile Magari madogo ya kubeba mizigo, pikipiki, bajaji, Mabasi, Malori, Trekta, Mashine za Uchimbaji na mengineyo ambayo yamesajiliwa kwa matumizi ya Kibiashara na Binafsi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Uzinduzi huo Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha Tigo Pesa, Angelica Pesha amesema kuwa lengo lao ni kutoa huduma ya bima kidigitali kwa watanzania waliowengi.

“Takriban watu milioni 53.18 wanapata huduma za simu za mkononi nchini Tanzania lakini ni asilimia 13 tu ya watu wote wanapata huduma za Bima. Lengo letu ni kuendeleza huduma za bima ya kidijitali kote nchini, hasa kwa wale ambao wamepata ugumu wa kufikia huduma hizi kupitia njia zilizozoeleka.

“Sekta ya Bima Tanzania inaendelea kuonyesha fursa nyingi za upanuzi na ukuaji, hii imejidhihirisha kupitia ongezeko la Taasisi mbalimbali zinazojihusisha na utoaji wa Bima ambalo lina uwezekano wa kuongeza mahitaji ya bidhaa za bima kidigitali kupitia simu ya mkononi, na sisi kama kampuni inayojali wateja wake ndio maana tukaamua kuja na TIGO MOTOR INSURANCE,”amesema Pesha.

Aidha, ameongeza kuwa: “Ushirikiano wetu na bima ya Milembe (MILEMBE INSURANCE) unalenga kuziba pengo la upatikanaji wa huduma za bima kwa kutoa suluhisho la kidijitali ambalo litapunguza gharama na kuongeza upatikanaji wa bidhaa za bima. Tunaamini kuwa zaidi ya wateja milioni 9 wa Tigo Pesa watatumia Huduma hii mpya ya bima, ambayo inapatikana kwa urahisi na gharama nafuu kabisa tena Kidigitali,”amesema Pesha.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu kutoka Milembe Insurance, Muganyizi Tibaijuka, amesema kuwa wanatarajia kuona ushirikiano huo ukiwawezesha kuwafikia Watanzania wengi zaidi.

“Bima ya Milembe wakiwa waanzilishi wa huduma ya Bima za Kidigitali nchini Tanzania maarufu kama BimaPap wana imani kuwa, kushirikiana na Tigo kunathibitisha kuwa ni hatua nyingine katika kuboresha ufanisi wa utendaji kazi na uhakikisho wa utoaji wa huduma bora kwa umma, hivyo basi kwa sasa wateja wa Tigo Pesa watapata unafuu wa kuvibimia vyombo vyao vya usafiri na kupewa Hati muhimu za Bima zao papo hapo kupitia simu zao.

“Aidha katika tukio la ajali ya gari ikiwa itawekewa bima kupitia Tigo Pesa, Mteja atatakiwa kuwasilisha taarifa ya madai kidigitali pasipo kulazimika kutembelea ofisi zetu na madai yake yataanza kushughulikiwa, hii inadhiirisha mustakabali mzuri kati ya Bima yetu na wateja wa Tigo Pesa,” amesema Tibaijuka.

Kwa mujibu wa Tigo. ili mteje aweze kupata huduma hiyo anaweza kusajili magari yao na kulipia BIMA kupitia MENU ya Tigo Pesa 15001#, chagua (7) huduma za kifedha, chagua (3) bima, chagua (2) bima ya magari, chagua (1) usajili wa gari, ingiza usajili wa gari. nambari, chagua (1) thibitisha na ujiandikishe, chagua (1) lipa, chagua matumizi ya gari, chagua (1) endelea kulipa, kisha weka pin ya Tigo Pesa ili kuthibitisha malipo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles