24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Tigo, BOA waja na huduma mpya

Na Beatrice Kaiza,Mtanzania Digital

KAMPUNI ya simu Tanzania ya Tigo kwa kushirikiana na Benki ya Afrika(BOA Tanzania), wamezindua huduma mpya ya kuhifadhi fedha kwa kutumia simu ya mkononi  inayoitwa “Tigo Pesa Kibubu” itakayowawezesha wateja wa kutunza fedha

Huduma hiyo itakayounganishwa kupitia akaunti kuu ya Tigo Pesa ambapo mtumiaji ataweza kuhifadhi fedha zake kidogo kidogo kuanzia sh. 1 na  kupata gawio pale atakapohifadhi kwa matumizi ya baadae.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 2, katika uzinduzi wa huduma hiyo, Ofisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Angelica Pesha, amesema  wamefanya hivyo kutokana na  kuongezeka kwa idadi ya Watanzania hasa ambao wanafanya miamala na kufanya huduma mbalimbali za kifedha kupitia Tigo Pesa.

“Takwimu zinaonesha kuwa watumiaji wa Tigo Pesa wameongezeka hadi kufikia millioni 9 nchi nzima na sisi kwa kushirikiana na BOA kwa kuwajali wateja wetu  tukaamua kuwaletea huduma hii ya TIGO PESA KIBUBU ili wafurahie kuhifadhi pesa zao kidigitali kwa ajili ya matumizi ya baadae huku wakipata gawio kulingana na kiasi cha Pesa watakachohifadhi.

“Huduma hii inaruhusu wateja wa Tigo Pesa kuhifadhi pesa na kupata gawio kulingana na salio liliopo. Gawio linalopatikana kila siku litakusanywa na kulipwa kila mwezi kulingana na salio ambalo litabaki kwenye mkoba wa mteja wa Tigo Pesa Kibubu,”amesema Pesha.

 Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa BOA, Wasia Mushi, amesema wanajivunia kushirikiana na Tigo katika kuwapelekea huduma mamilioni ya wananchi hasa ambao wako nje ya mfumo rasmi wa kibenki.

“Ni matumaini yetu kuwa huduma hii itarahisisha maisha na kukuza ujumuishaji wa kifedha, benki kwa kushirikiana na Tigo tutakuwa msitari wa mbele kuhakikisha huduma hii inafanikiwa,” anasema .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles