Kulwa Mzee, Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando amedai mchakato wa kulitoa shirika hilo analogia kuingia kwenye digitali ulitokana na maelekezo ya Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete.
Amedai hatua hiyo ilitokana na uamuzi wake wa kumtaka alibadilishe shirika lifikie katika hadhi inayostahili ambapi pia mchakato huo ulifanywa na Bodi ya shirika hilo na kupata baraka za Bodi ya Zabuni.
Tido amedai hayo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Alhamisi Septemba 20, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi alipokuwa akijitetea kuhusiana na tuhuma zinazomkabili akiongozwa na Wakili wake, Dk. Ramadhani Maleta.
Mshtakiwa huyo anakabiliwa na mashtaka manne yakiwamo kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh milioni 887.1.