29.1 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

TIC: UWEKEZAJI UNAIMARIKA NCHINI

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


MKURUGENZI  Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Geoffrey Mwambe, amesema uwekezaji unazidi kushamiri nchini Tanzania na TIC inahakikisha wawekezaji wanaendesha shughuli zao vizuri na kwa faida.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwambe alisema kwa sasa TIC imeondoa dosari zote zilizokuwa zinawakwaza wawekezaji na kwamba mwekezaji mpya anakamilisha mchakato wote wa kupata vibali na nyaraka nyingine za kumwezesha kuwekeza ndani siku tatu na kila huduma inapatikana ndani ya Ofisi ya TIC (One Stop Center).

Mkurugenzi huyo alipinga madai ya baadhi ya taarifa zinazodai hali ya uwekezaji Tanzania ni mbaya kwa kusema kuwa huo ni uzushi wenye nia ya kuchafua sifa ya Tanzania ambayo kwa ni moja ya nchi 10 zenye uchumi unaokuwa kwa kasi zaidi duniani kwa wastani wa asilimia 7.2, na ni nchi inayoongoza kwa uwekezaji Afrika Mashariki.

“Ndani ya kipindi cha miaka miwili Tanzania imepata uwekezaji wa Dola za Marekani Bilioni 1.35 sawa na zaidi ya Sh trilioni 3, ikifuatiwa na Uganda iliyopata uwekezaji wa Dola za Marekani milioni 537 ambao ni chini ya nusu ya Tanzania.

“Pamoja kuwepo kwa hali nzuri ya uwekezaji TIC inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuwavutia wawekezaji na kuwaeleza fursa mbalimbali muhimu ikiwemo uwepo wa soko la uhakika la ndani ya nchi na nje ya nchi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles