27.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

THRDC yawalilia wafugaji

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) umesema kuna ukiukwaji wa haki za mifugo katika maeneo mbalimbali nchini ambako imekuwa ikikamatwa, kuuzwa ama kutaifishwa.

Akizungumza leo Novemba 8,2023 wakati akitoa tamko lililoandaliwa na mashirika 16 kuhusu sakata hilo, Mkuu wa Idara ya Utetezi THRDC, Wakili Paul Kisabo, amesema kumekuwa na kutokuheshimiwa kwa amri za mahakama na kusababisha mifugo kuuzwa kinyume cha sheria.

Ametoa mfano kuwa Oktoba 31,2023 Serikali ilifungua kesi namba 1 ya mwaka 2023 katika Mahakama ya Wilaya ya Ngorongoro ili kutaifisha mifugo iliyokamatwa katika eneo ambalo amedai kuna zuio la mahakama kuu.

Mkurugenzi wa Jukwaa la Katiba Tanzania(JUKATA), Bob Wangwe, akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa tamko lililoandaliwa na mashirika 16.

“Ingawa Serikali iliondoa kesi hiyo mahakamani lakini maofisa wa wanyamapori wamekataa kuachia mifugo hadi ilipwe faini ya Sh 100,000 kwa kila ng’ombe.

“Vitendo hivi si tu vinakiuka haki za mifugo, haki za binadamu na katiba ya nchi yetu lakini pia ni shambulio kwa uhuru wa mahakama na utawala wa sheria nchini. 

“Tunatoa wito kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwaelekeza watumishi wa Serikali hasa katika maeneo lalamikiwa kuheshimu maamuzi na amri za mahakama kwani zinapaswa kuheshimiwa na kila mtu,” amesema Kisabo.

Mtandao huo pia umetoa wito kwa mahakama kufuatilia utekelezaji wa maamuzi yake kwani wanaamini ni maamuzi ya haki hivyo yanapaswa kutekelezwa na kila mtu kama yalivyoamuliwa.

Naye Mkurugenzi wa Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA), Bob Wangwe, ameshauri Serikali ifanye tathmini ya athari zilizofanyika mpaka sasa na hatua zichukuliwe dhidi ya wahusika.

“Bunge lichukue hatua kuhakikisha linalinda masilahi na maisha ya wananchi na wafugaji…tunahitaji bunge lijadili jambo hili,” amesema Wangwe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles