21.2 C
Dar es Salaam
Sunday, August 14, 2022

Thierry Henry kocha mpya Montreal Impact

MONTREAL, CANADA

ALIYEKUWA kocha wa timu ya Monaco, Thierry Henry, ametangazwa kuwa kocha mpya wa timu ya Montreal Impact ambayo inashiriki Ligi nchini Marekani.

Henry aliwahi kuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa Ubelgiji wakati wa michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi huku kocha mkuu akiwa Roberto Martínez.

Kocha huyo aliwahi kuwa staa ndani ya klabu ya Arsenal pamoja na timu ya taifa ya Ufaransa, hivyo amesaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili hadi 2022.

Kocha huyo wakati anaisimamia timu ya taifa Ubelgiji chini ya Martinez, aliweza kuisaidia timu hiyo kumaliza nafasi ya tatu kwenye Kombe la Dunia, lakini baada ya hapo akasaini mkataba na Monaco, Octoba 2018.

Lakini wakati anaisimamia timu hakuweza kuonesha uwezo wake ndani ya viwanja vya Stade Louis II, hivyo akafungashiwa virago Januari 24 mwaka huu huku akishinda michezo minne kati ya 20 aliyoisimamia.

Hivyo uongozi wa Montreal umeona bora umpe nafasi hiyo kwa ajili ya kuonesha uwezo wake kocha huyo mwenye umri wa miaka 42.

“Tunatumia nafasi hii kutangaza kuwa gwiji wa soka tuko naye kwenye kikosi chetu, huyu ni Thierry Henry, tunaamini anakuja kwa ajili ya kuibadilisha klabu yetu, yupo tayari kuungana na sisi kwenye mtazamo wetu juu ya timu yetu.

“Hivyo tunaamini lengo letu litakamilika hasa katika kutimiza yale ambayo yapo kweny mifumo yetu, yeye ni mshindani mkubwa na kiongozi kwenye timu ambaye amewahi kucheza soka katika hatua ya juu kwenye maisha yake ya soka, hivyo tunaamini kutakuwa na mabadiliko makubwa kwenye timu yetu,” alisema rais wa timu hiyo Kevin Gilmour.

Kwa upande mwingine Henry amedai kuwa na furaha kupata nafasi hiyo kwa kuwa ni Ligi ambayo ana uzoefu naye baada ya kuwa mchezaji wa timu ya New York Red Bulls kwa kipindi cha miaka minne, hivyo anaamini atafanya makubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,656FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles