26.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 26, 2023

Contact us: [email protected]

THIERRY HENRY AMVUTA JOKATE ARSENAL

MSANII wa muziki na mwanamitindo nchini, Jokate Mwegelo, ametangaza kuwa shabiki mpya wa klabu ya Arsenal, baada ya kukutana na mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo na timu ya Taifa ya Ufaransa, Thierry Henry, nchini Afrika Kusini.

Wawili hao wamekutana kwenye mchezo wa kikapu wa NBA Africa Game nchini humo mwishoni mwa wiki iliyopita na kupata chakula cha pamoja.

Jokate alitumia akaunti yake ya Instagram kuposti picha akiwa na mchezaji huyo, kisha kuweka wazi kuwa anahamia klabu hiyo ya Arsenal.

“Furaha kubwa kula chakula na Thierry Henry kabla ya kuanza kwa mchezo wa NBA Africa Game, kuanzia sasa ninahamia rasmi klabu ya Arsenal, naomba ushauri kwa kuwa ninaambiwa kuishabikia timu hiyo unatafuta mawazo,” aliandika Jokate.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,726FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles