30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 30, 2023

Contact us: [email protected]

Thierry Henry aanza kukinoa kikosi cha Ubelgiji

Training National Soccer Team of Belgium - 29082016

BRUSSELS, UBELGIJI

KOCHA msaidizi wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Thierry Henry, ameanza kazi rasmi ya kukinoa kikosi hicho kwa ajili ya michuano ya kufuzu Kombe la Dunia 2018.

Henry ameanza kazi Jumatatu wiki hii akiwa na mastaa wa timu hiyo ambao wanafanya vizuri katika Ligi ya England na sehemu zingine walizoungana kwa ajili ya kuitumikia timu yao.

Kabla ya kuanza kwa mazoezi, kocha huyo alikutana na wachezaji wake katika hoteli jijini Brussels na kuanza kujitambulisha mbele yao.

“Hallo mimi ni Thierry Henry, nipo hapa kwa ajili ya kuwa kocha msaidizi, hivyo ninahitaji ushirikiano wenu kuweza kutimiza malengo ya timu hii,” alisema Henry mbele ya nyota wake kama vile Eden Hazard, Romelu Lukaku, Michy Batshuayi, Divock Origi na Christian Benteke.

Henry amepewa nafasi hiyo ya kuwa kocha msaidizi chini ya kocha mkuu, Roberto Martinez, ambaye alikuwa anaifundisha klabu ya Everton ya nchini England, ila kwa sasa anakinoa kikosi hicho cha Ubelgiji.

Kikosi hicho kimeanza mazoezi kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Hispania ambao utapigwa kesho nchini humo kabla ya mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Cyprus, Septemba 6, wakiwa ugenini.

Baada ya kumalizika kwa mazoezi hayo, kocha Martinez alionekana kutumia muda wake kufanya mazungumzo na Henry huku wachezaji wakiwa wanawasubiri kwa ajili ya kufanya mazungumzo nao.

Martinez alianza kwa kusema: “Tayari kila mmoja amejitambulisha, lakini kikubwa ambacho kimetuleta hapa ni kujiandaa na mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia, nipo na Henry tunaamini tutafanikisha hilo.

“Henry ana uzoefu wa michuano mikubwa na anawajua wachezaji wengi, hivyo kutokana na uwezo wake, ninaamini ataisaidia timu hii kutimiza malengo katika michuano mikubwa,” alisema Martinez.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles