The Rock aanika kilichomuua baba yake

0
711

New York, Marekani

STAA wa filamu nchini Marekani, Dwayne Johnson, maarufu kwa jina la The Rock, ameweka wazi chanzo cha kifo cha baba yake aliyepoteza maisha mwishoni mwa wiki iliopita.

Taarifa za awali hazikuweka wazi chanzo cha kifo hicho, lakini msanii huyo ametumia ukurasa wake wa Instagram na kuweka wazi chanzo cha kifo hicho kuwa ni mshtuko wa moyo.

“Kama mnavyojua nimempoteza baba yangu siku chache zilizopita, ndio hiyo nimempoteza na wala sikupata nafasi ya kuagana naye, sikupata hata muda wa kumkumbatia na kumwambia neno la kumshukuru kwa kile alichokifanya katika maisha yangu.

“Najua wengi wanataka kujua chanzo cha kifo hicho, ukweli ni kwamba alikuwa hajisikii vizuri, mara zote alikuwa analalamika juu ya baridi, lakini kilichopoteza uhai wake ni shambulio la moyo,” alisema msanii huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here