The Game kuachia albamu ya mwisho

0
689
NYOTA wa muziki wa hip hop nchini Marekani, The Game

NEW YORK, MAREKANI

NYOTA wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Jayceon Taylor, anayejulikana kwa jina la The Game, amesema albamu yake ya mwisho ‘Born 2 Rap’ anatarajia kuiachia Novemba mwaka huu.

Albamu hiyo itakuwa ya tisa kwa msanii huyo huku ikiwa ya kwanza tangu mwaka 2016. Mapema mwaka huu alisema albamu hiyo ataiachia Okotoba, lakini ilipofika Agosti akabadilisha maamuzi na badala yake akaachia wimbo uliojulikana kwa jina la Mad Max.

“Kwa marafiki zangu tangu siku ya kwanza na wale wote ambao wanasubiri albamu yangu mpya, najua nimekuwa kimya kwa muda mrefu bila kuelezea habari hii, sasa ni wazi kuwa albamu hiyo itakuwa tayari Novemba,” aliandika The Game.

Ujumbe huo aliuweka kwenye ukurasa wake wa Instagram ambao una wafuasi milioni 11. Hata hivyo hakuweka wazi kama huo ni mwisho wake wa kufanya muziki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here