TGNP: Bajeti ya maji vijijini isipunguzwe

0
260

KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

TGNP Mtandao imependekeza katika utekelezaji wa bajeti, bajeti ya maji vijijini isipunguzwe kwa sababu ni muhimu kwa ajili ya kumpunguzia mzigo mwanamke.

Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Mtandao, Lilian Liundi amesema hayo katika mjadala wa makadirio ya Bajeti ya mwaka 2020/2021 kwa mrengo wa jinsi.

Pamoja na mambo mengine alizungumzia suala la maji na kubainisha kwamba siku za nyuma miradi ya maji ilikuwa na changamoto kubwa, fedha za wafadhili zilikuwa zinaliwa lakini tangu Rais John Magufuli aingia madarakani changamoto hiyo imeshughulikiwa na mafanikio makubwa yanaonekana.

“Tunapendekeza bajeti ya maji vijijini isipunguzwe kwani ni muhimu kwa ajili ya kumpunguzia mwanamke mzigo.

“Shule nyingi na baadhi ya vituo vya afya vijijini havina maji, wananchi hao wanahitaji pia wapate maji safi na salama,”alisema.

Pia amependekeza badala ya kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake watano watano wapewe vifaa vya teknolojia kama mashine ili waweze kuzalisha kuinua vipato vyao.

Ameziomba Benki za kilimo kuliangalia hilo kwa lengo la kuwainua wanawake kiuchumi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here