26.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

TFS yatakiwa kutengeneza mizinga ya nyuki

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) umeagizwa kutengeneza mizinga ya nyuki na kuitoa kwa wananchi ili kuwajengea utaratibu wa ufugaji nyuki, hatua ambayo itatapunguza ukataji miti holela.

Aidha, imetakiwa kuunganisha nguvu na Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB)hatua itakayosaidia kutangaza vivutio vya misitu vilivyopo nchini.

Hayo yamebainishwa Julai 11, jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja baada ya kutembelea banda la Maliasili na Utalii lililopo katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yatakayohitimishwa Julai 13, mwaka huu.

Amesema TFS isiishie kuhifadhi misitu bali itumie fursa hiyo ambayo itawezesha kuzalishwa kwa asali kwa wingi na kutoa ajira kwa walio wengi lakini pia kuwafanya wananchi kuona faida kwenye misitu.

“Msiishie tu kuwa na siku ya nyuki duniani, sisi ndio wa kuwafanya wananchi waone umuhimu wa misitu, mizinga hiyo iwe ya mfano na wananchi watakapoona kuna faida wengi wataiga hivyo msikae kimya,”amesema Masanja.

Akizungumzia kutangaza vivutio vya misitu, amesema kama ambavyo kazi ya Wakala huo ni kuhifadhi misitu, wana wajibu wa kushirikiana na TTB ili kutangaza vivutio vya misitu na kuongeza watalii.

“Kuweni karibu na TTB kazi yao kubwa ni kutangaza utalii pamoja na kuwa tunahifadhi misitu fanyeni kazi kwa pamoja utalii utakuwa mno,wekezeni hata katika mashamba kwa mpangilio mzuri nao ni utalii na unganishe nguvu,” amesema Masanja.

Amesema utalii siyo wanyamapori tu bali ni pamoja na utalii wa ikolojia ambao unavuna hewa safi tofauti na nyingine, mali kale na magofu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles