24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

TFS yashauri umwagiliaji wa miti kutunza mazingira

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Wakala wa Huduma za Misiti (TFS) Kanda ya Kati wameshauri kuwe na utaratibu wa kumwagilia miti hususan kipindi cha kiangazi lengo likiwa ni kuendelea kutunza na kuhifadhi mazingira.

Hayo yameelezwa leo Ijumaa Februari 11, 2022 na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi kutoka  TFS Kanda ya Kati, Mathew Kiondo wakati akizungumza na wanafunzi na wananchi walioshiriki zoezi la kupanda miti katika eneo la Tambukareli mkoani Dodoma.

Kiondo ametaka miti hiyo kutunzwa baada ya msimu wa mvua kuisha na kudhibiti mifugo lengo likiwa ni kutunza mazingira.

“Si vizuri tukapanda miti leo halafu mwakani tena tunapanda sehemu hii hii, tutakuwa tunapoteza nguvu na fedha za Serikali kwa hiyo tuhakikishe tumepanda leo, tuite mkutano kama huu kuja kumwagilia maji kwa kuwa Dodoma kipindi cha ukame ni kirefu,”amesema Kiondo.

Kwa upande wake Balozi wa Mazingira na Mbunge wa Pandani, Mariam Omary Saidi, amewataka wakazi wa Dodoma kuhakikisha wanaitunza miti na mazingira ili kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.

Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango anatarajiwa kuzindua Sera mpya ya Taifa ya Mazingira ya Mwaka 2021 utakaofanyika kesho Februari 12,2022 jijini Dodoma.

Hayo yameelezwa leo na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mary Maganga, wakati akiwaongoza wanafunzi na wananchi walioshiriki zoezi hilo la upandaji miti.

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mary Maganga.

Katibu Mkuu huyo amesema kuwa katika wiki hiyo wananchi wamehamasika na kujitokeza kufanya shughuli mbalimbali zilizopangwa ikiwamo kupanda miti na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali.

“Kila tulipokwenda kwa ajili ya kupanda miti tunakuta umati mkubwa wa watu, mwamko ni mkubwa na watanzania wamehamasika na  kesho ni kilele cha shughuli hii yote tunahitimisha kwa kuzindua sera mpya ya mazingira,”amesema Maganga

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles