25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

TFS, Magereza wapanda miti 1,300 kusheherekea uhuru

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imeshirikiana na Jeshi la Magereza, wadau wa mazingira pamoja na Miss Tanzania, Rose Manfere wameadhimisha sherehe za Uhuru kwa kupanda miti katika gereza la Wazo Hill jijini Dar es Salaam.

Shughuli hiyo imefanyika leo Desemba 9, katika shamba la gereza hilo, ikiongozwa na Meneja Rasilimali Misitu Tanzania, Dk. Abel Masota pamoja Mkuu wa Gereza la Wazo Hill Ipyana Mwakyusa, wadau wa mazingira na waratibu wa Miss Tanzania.

Dk. Masota alisema Serikali imeagiza sherehe za Uhuru zitumike katika kufanya shughuli za kijamii na wao wameamua kupanda miche 1,300 kati ya hiyo 1,000 ya misaji ambayo inatoa mbao ngumu na iliyobaki ya matunda mbalimbali.

“Tukishirikiana na uongozi wa magereza, wadau wa mazingira na Kamati ya Miss Tanzania tumeamua kupanda miche hii ya misaji ili siku za usoni iende kuwasaidia wenzetu katika shughuli zao za ujenzi hata biashara. Serikali ina mashamba mawili ya misaji ambayo huuza miti kwa njia yam nada kila mwezi na sehemu kubwa ya wanunuzi wa mazao haya husafirisha nje ya nchi.

“Thamani ya miche hii ikikuua ni kubwa sana tuna imani itawanufaisha jeshi la magereza. Tumeona magereza wana eneo kubwa kupanda miche hii na ni wajibu wao sasa kuitunza vizuri kwa manufaa ya baadaye,” amesema Dk. Masota.

Katika hafla iliyoshirikisha wananchi mbalimbali, mtaalam huyo wa masuala ya misitu alitumia nafasi hiyo kutoa elimu ya namna ya hatua zinazotakiwa kufuatwa katika upandaji wa miche hadi kustawi.

Miss Tanzania Rose amesema kupitia shughuli amejifunza namna ya kupanda miti na hatua zinazotakiwa kufuatwa huku akiwataka wananchi kujenga utamduni wa kuithamini misitu.

“Sijawahi kupanda mti hii ni fursa kwangu, leo nimejifunza vitu vingi kupitia shughuli hii. Nimejifunza namna ya kupanda miche, kuitunza hadi kuivuna,” amesema Rose ambaye aliambatana na mratibu wa mashindano ya Miss Tanzania, Basila Mwanukuzi.

Naye, Mkuu wa gereza hilo, Mwakyusa amesema kitendo cha uongozi wa TFS kupanda miche hiyo katika shamba lao ni fursa kwao huku akiahidi kuitunza vyema ili iwaletee manufaa kwa siku za baadaye.

“Hapa tuna wataalamu wa kilimo na mifugo tutahakikisha tunaisimamia ipasavyo ikiwemo kuitunza na kuimwagilia lengo ni kuhakikisha inatusaidia kwa siku za usoni baada ya kukua,” amesema.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Stellah Msophe amesema Katika Miche 1,300 iliyopandwa ana imani itakuwa sehemu kubwa ya kuboresha mazingira na kama Wilaya wataendelea kuwaunga mkono TFS kwenye uhamasishaji wa upandaji miti.

“Tunashukuru Miss wetu umefika hapa kupanda miti na sisi na hii ikawe chachu kwa vijana popote walipo wapande miti lakini niwataka magereza kuhakikisha miti hii inakuwa kwani nguvu kazi mnayo ili kesho tusione aibu kuwaomba TFS watusaidie tena na tena kuotesha miti,” amesema Stellah.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles