31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

TFDA yavuka malengo walojiwekea

Ferdnanda Mbamila, Dar es Salaam

Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA), imefanikiwa kufikia na kuvuka malengo iliyojiwekea katika udhibiti wa ubora, usalama na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi ili kulinda afya ya jamii.

Mafanikio hayo ya TFDA yametokana na  kuweka mifumo na taratibu za ndani za utoaji huduma bora kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya ‘ISO 9001:2015’ kwa huduma za kawaida na ‘ISO 17025:2005’ kwa huduma za maabara.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam Desemba 31, na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Adam Mitangu wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa kazi za udhibiti wa ubora, usalama na ufanisi wa bidhaa chini ya serikali ya awamu ya tano.

Amesema mfumo wa usajili wa bidhaa umeendelea kuimarika ambapo idadi ya bidhaa za chakula,dawa, vipodozi,vifaa tiba na vitendanishi imekua ikiongezeka mwaka hadi mwaka,katika kipindi cha mwaka 2015/16 hadi 2017/18.

”TFDA imesajili jumla ya bidhaa 14,345 kutoka bidhaa 8,866 zilizokuwa zimesajiliwa mwaka 2015/16 ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 62 na hii imetokana na kuongezeka kwa uelewa wa matakwa ya sheria miongoni mwa wafanyabiashara na kukua kwa biashara,”amesema Fimbo.

Amesema TFDA imeweka mifumo ya utoaji wa huduma kwa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) ambapo taarifa na takwimu  zikiwamo za bidhaa na majengo yaliyosajiliwa na zile za wateja zimewekwa katika mfumo maalumu uitwao ‘IMIS’ ambao isisha utoaji huduma kwa wateja kwani wanaweza kulpeleka maombi yao kwa mtandao bila kufika ofisi zao.

”Ukuaji wa viwanda vya ndani na uwezeshaji wa wasindikaji wa chakula katika jitihada za kujenga Tanzania ya viwanda ifikapo 2025, TFDA imekua mstari wa mbele katika kutoa msaada wa kiufundi na kuwajengea nchini na kushawishi wawekezaji kujenga viwanda vya dawa,”alisema Fimbo.uwezo wenye viwanda vya dawa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles