23.8 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

Tetesi za Soka Ulaya

Dembele anukia mkataba Barca

BARCELONA wako mbioni kumpa mkataba mpya mshambuliaji wake raia wa Ufaransa, Ousmane Dembele, licha ya huu wa sasa kubakiza mwaka mmoja.

Dembele (24), amekuwa akisumbuliwa na majeraha na hata kuhusishwa na mlango wa kutokea Camp Nou.

Lakini sasa, imefichuka kuwa mkataba huo utakwenda sambamba na punguzo la mshahara wa mchezaji huyo.

Dembele aliyemaliza msimu wa La Liga akiwa na mabao sita, bado hajazungumzia ofa hiyo ya Barca.

Kocha Ureno kutua Wolves

WOLVES wameanza mazungumzo na kocha Bruno Lage ili akalie kiti kilichoachwa wazi na Nuno Espirito Santo.

Lage (45), aliwahi kuinoa Benfica na pia anaijua England kwani alikuwa kocha msaidizi pale Swansea na Sheffield Wednesday.

Akiwa na Benfica, itakumbukwa kuwa kocha huyo aliipa ‘ndoo’ ya Ligi Kuu mwaka juzi, kabla ya kuondoka miezi 12 baadaye.

Ifahamike kwua wakala wake ni Jorge Mendes, ambaye pia ndiye anayemsimamia kocha aliyeondoka Wolves, Nuno.

AC Milan kubeba kipa Lille

KLABU ya Lille imepanga kumsajili mlinda mlango wa Lille ya Ufaransa, Mike Maignan.

Milan wanaamini kipa huyo ndiye mrithi sahihi wa kipa wao anayetaka kuondoka, Gianluigi Donnarumma.

Maignan (25), ndiye aliyekuwa langoni kwa mechi za Lille katika safari ya timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligue 1 msimu huu uliokwisha hivi karibuni.

Kipa huyo alikuwa jijini Milan jana na imeelezwa kwamba atasajiliwa kwa Pauni milioni 15.

Ronaldo kumbe haondoki Juve

STAA wa Juventus, Cristiano Ronaldo, yuko mbioni kuanza mazungumzo ya mkataba mpya na Juventus.

Ronaldo (36), amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na zilikuwapo tetesi kuwa atatimka mwishoni mwa msimu huu.

Taarifa za Ronaldo kuondoka Juve zilizi kusambaa baada ya Juve kumaliza msimu ikiwa nafasi ya nne kwenye msimamo wa Serie A.

Ukiacha Real Madrid, ilielezwa kuwa mkali wa mabao huyo angerejea England na kujiunga na Manchester United.

Ceballos: Naondoka Arsenal

BAADA ya misimu miwili ya kucheza kwa mkopop akitokea Real Madrid, kiungo Dani Ceballos amesema atatimka Arsenal.

Huku ikielezwa atarudi Madrid, Ceballos amefunga mabao mawili tu na kutoa ‘asisti’ tano kwa kipindi chote alichokaa Emirates.

Huenda Ceballos amefikia uamuzi huo baada ya Arsenal kumaliza msimu huu ikiwa nafasi ya nane, hivyo kuikosa michuano yote ya Ulaya msimu ujao.

Pigo jingine kubwa kwa Washika Bunduki msimu huu ni kuishia nusu fainali ya Ligi ya Europa, safari yao ikikwamishwa na Villarreal.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,248FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles