28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Tetesi za Soka Ulaya

Dortmund: Sancho nenda zako

BORUSSIA Dortmund wamempa ruhusa ya kuondoka klabuni hapo winga wao raia wa England, Jadon Sancho.

Hii ni habari njema kwa kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, ambaye amekuwa akimtamani mchezaji huyo.

Taarifa zinadai Solskjaer ameamua kumfungia kazi Sancho na kuachana na kuachana na kiungo wa Aston Villa, Jack Grealish.

Lakini sasa, baadhi ya wachezaji wa Man United wanamwambia kocha huyo amchukue Grealish badala ya Sancho.

Pochettino atajwa Tottenham

BAADHI ya vigogo ndani ya Tottenham wameanza kuwashaiwshi wenzao kumrejesha kocha Mauricio Pochettino.

Tottenham hawana kocha mkuu tangu Jose Mourinho alipoondoka na Pochettino kwa sasa anainoa PSG.

Sasa, imeelezwa kuwa hata Mwenyekiti wa klabu hiyo, Daniel Levy, naye ameanza kuona umuhimu wa kumwajiri tena Muargentina huyo.

Aidha, Pochettino aliyeondoka Tottenham mwaka juzi, naye yuko ametajwa kufungua mlango wa kurudi klabuni hapo.

Madrid: Anayemtaka Bale aje tu

REAL Madrid iko tayari kusikiliza ofa ya klabu yoyote inayomtaka winga wake raia wa Wales, Gareth Bale.

Wakati huo huo, Madrid wako tayari kumpiga bei kiungo wake raia wa Ubelgiji, Eden Hazard.

Taarifa zimedai Madrid inataka wawili hao waondoke ili iwasajili Kylian Mbappe na Erling Haaland.

Kwa upande wake, Hazard aliyeifungia Madrid mabao matano tu tangu asajiliwe mwaka juzi, anataka kurejea Chelsea.

Suarez kubaki Atletico

STAA wa Atletico Madrid, Luis Suarez, amesema hatawakacha mabingwa wapya wa La Liga, Atletico Madrid.

Suarez (34), anayasema hayo huku akihusishwa na Liverpool na klabu mbalimbali za Ligi Kuu ya Marekani.

Alipoulizwa juu ya uwezekano wa kubaki Atletico, amejibu: “Ndiyo, nina uhakika (wa kubaki).”

Raia huyo wa Uruguay amemaliza msimu uliokwisha hivi karibuni akiwa na mabao 21, likiwamo la ushindi katika mchezo uliowapa ndoo ya La Liga.

Ramsey awekwa sokoni Juventus

KLABU ya Juventus imesema iko tayari kumpiga bei kiungo wake mwenye umri wa miaka 30, Aaron Ramsey.

Ramsey ameshindwa kung’ara Juve kwani amecheza mechi 65 tu tangu atue klabuni hapo akitokea Arsenal mwaka juzi.

Tottenham na Everton zimekuwa zikiifukuzia saini yake, ingawa pia kuna ofa kutoka Inter Miami ya Marekani.

Katika hatua nyingine, Ramsey aliweka wazi ndoto yake ya kuvaa kwa mara nyingine jezi ya Arsenal.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,303FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles