30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Tetesi kubuniwa chama kipya zaitikisha Jubilee

ISIJI DOMINIC

Sintofahanu ndani ya chama tawala cha Jubilee kimechukua sura mpya baada ya tetesi ya kusudio ya kuanzisha chama kingine kipya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2022.

Ikumbukwe kuwa Jubilee ilibuniwa baada ya takribani vyama 13 kuvunjwa huku vyama viwili vikubwa vikiwa ni TNA chini ya Rais Uhuru Kenyatta na URP iliyoanzishwa na Naibu Rais William Ruto kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2013.

Hata hivyo katika siku za hivi karibuni, Jubilee imekuwa katika mtikisiko hususan baada ya Rais Uhuru kuanza kufanya kazi akishirikiana na hasimu wake kisiasa ambaye pia ni kinara wa upinzani, Raila Odinga.

Kitendo hicho kimeonekana kuwaghadhabisha baadhi ya wanachama wanaomuunga mkono Ruto ambao wamekuwa wakidai makubaliano ya awali ni kwamba Rais Uhuru atakapomaliza muda wake wa uongozi atampigia debe Naibu Rais Ruto kuridhi mikoba yake. Aidha wanaona ujio wa Raila unamweka Ruto katika wakati mgumu kisiasa.

Licha ya Ruto mara kadhaa kusisitiza Chama cha Jubilee kiko imara, mvutano baina ya makundi mawili yaliyopachikwa majina ya ‘Tangatanga’ na ‘Kieleweke’ yanaonyesha picha tofauti. Tayari kulikuwa na tetesi ya kuzaliwa upya kwa chama cha URP chini ya Ruto na sasa kundi la wanasiasa kutoka Mlima Kenya wanataka kuanzisha chama cha Transformation National Alliance Party (TNAP).

Mwanasiasa anayehusishwa na chama hiki ni Mbunge wa Gatundu Kusini ambako anatokea Rais Uhuru, Moses Kuria, anayedai TNAP itatetea maslahi ya wakazi wa Mlima Kenya katika serikali zijazo. Kuria aliwahi kumshutumu Rais Uhuru kupeleka maendeleo maeneo ambayo hawakumpigia kura matamsha ambayo hayakupokelewa vyema na Rais na kusisitiza yeye ni Rais wa Kenya sio maeneo au kundi fulani la watu. 

Hata kabla chama kipya cha Kuria hakijapata usajili wa kudumu, tayari ameanza kupingwa vikali na wanasiasa wakitaja hatua yake kuirudisha nyuma eneo la Mlima Kenya na nchi kwa ujumla na anakumbatia vyama vya siasa vyenye mrengo wa kikabila.

Wabunge hao wengi kutoka Mlima Kenya ambao ni Peter Kimari (Mathioya), Ndindi Nyoro (Kiharu) na Kimani Ichungwa (Kikuyu) pamoja na Seneta wa Murang’a Irungu Kang’ata na magavana Ann Waiguru (Kirinyaga) na Mutahi Kahiga (Nyeri) walisisitiza watu kutoka Mlima Kenya watabaki ndani ya Jubilee.

Kang’ata alisema Kuria anahatarisha ‘kutupwa kwenye jangwa la kisiasa’ endapo hataachana na chama chake cha ‘kikabila’.

“Kama Kuria kweli anayonia ya kuwa rais wa nchi hii hana budi kuachana na chama chake ndogo na kurudi Jubilee ili awashawishi viongozi pamoja na mkoa kwanini anastahili kuwa mgombea urais kupitia chama cha Jubilee,” alisema Seneta huyo wa Murang’a.

Naye Gavana wa Kirinyaga, Ann Waiguru, alisema sio jambo jema kufafanua chama kwa misingi ya ukabila wakati viongozi wanahangaika kuwaunganisha wananchi na kujenga taasisi imara za kitaifa.

Alisema Jubilee inapitia kipindi kigumu ila anaamini haitayumbishwa 2022 na baada ya hapo, na kwamba matatizo ya sasa ndani ya chama ni ya kawaida katika mazingira ya kisiasa ya ushindani.

Gavana wa Nyeri, Mutahi Kahiga, naye hakukosa neno kumhusu Kuria akihoji ujasiri wake kuanzisha chama na kuongea kwa niamba ya viongozi wa Mlima Kenya huku akisisitiza chama hicho chake kitaungana na vyama vingi vilivyoanzishwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles