24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 26, 2022

TETEMEKO LA ARDHI LAUA 82 INDONESIA

JARKATA, INDONESIA


SERIKALI ya Indonesia imesema zaidi ya watu 82 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 10,000 wameokolewa, baada ya tetemeko kubwa la ardhi kukikumba Kisiwa cha Lombok kilichopo katika Jimbo la West Nusa Tenggara juzi.

Maofisa wa Idara ya Kudhibiti Majanga, walisema pia tetemeko hilo lenye nguvu ya vipimo vya Richter 7,  limeharibu vibaya miundombinu ya umeme, barabara na nyumba.

Katika kisiwa jirani cha Bali, picha za video zimeonyesha watu wakikimbia majumbani mwao huku wakipiga kelele kuomba msaada.

Tetemeko hili limekuja wiki moja baada ya jingine kupiga sehemu hiyo ya Lombok, kisiwa maarufu kwa shughuli za utalii na watu 16 walifariki dunia.

Tahadhari ya kuwapo kwa kwa kimbunga ilitangazwa kisiwani hapo, lakini ikaondolewa saa chache baadaye.

Msemaji wa Idara ya Kudhibiti Majanga nchini hapa,  alisema nyumba nyingi zimeathirika, na kati ya hizo nyingi zilijengwa kwa kutumia nyenzo duni.

Wakati tetemeko hilo likitokea, Waziri wa Mambo ya Ndani, Kasiviswanathan Shanmugam, alikuwa ziarani katika kisiwa hicho na alituma picha kwenye mitandao ya kijamii akionyesha namna chumba chake kilivyoathirika.

“Wakati natembea nilisikia mingurumo, taratibu, taratibu, baadaye ikawa mikubwa na watu wakaanza kukimbia wakisema ‘tetemeko’, kila mmoja wetu alichanganyikiwa na kutoka nje ya nyumba, maofisa usalama wakasema kila mtu atoke ndani,” alisema Shanmugam.

Daktari Ketut Sudartana wa Hospitali ya Sanglah mjini Bali, alisema kwamba waliamua kuwatibia wagonjwa nje ili kuhakikisha usalama wao.

“Kwa wakati huu tutawatibu wagonjwa hapa nje, na kwenye sehemu za wazi za kufanyia mazoezi. Tutaweka mahema ya dharura nje ya hospitali kuwahifadhi wagonjwa wote pale, ili madaktari na manesi wetu waweze kuwahudumia vizuri zaidi,” alisema.

Rais Joko Widodo, alisema Serikali yake inafanya jitihada za kutosha kunusuru maisha ya majeruhi, huku akituma salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,051FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles