25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

TET, Unesco zatoa mafunzo stadi za maisha

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), zinaendesha mafunzo ya ujaribishaji wa Miongozo ya Elimu ya Stadi za Maisha kwa walimu wa shule za Msingi na Sekondari nchini.

Mafunzo hayo yanayofanyika Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, yamezinduliwa leo Juni 14, 2021 na Mkurugenzi wa Mafunzo ya Mitaala wa TET, Fika Mwakabungu.

Akizungumza katika ufunguzi huo mkurugenzi huyo amesema walimu 1,696 katika halmashauri 13 nchini watapatiwa mafunzo hayo na kisha wataweza kuwafundisha wenzao ili wakatoe uelewa wa stadi za maisha.

“Karne hii ya 21 wanafunzi wanapaswa kuandaliwa mapema kwani wanakutana na mambo mengi hivyo tunapowaandaa mapema kujua masuala mbalimbali wataweza kuepukana na changamoto zinazowakabili,” amesema Fika.

Mafunzo hayo ya stadi za maisha yanahusisha masuala ya afya, afya ya uzazi, Virusi Vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi na jinsia, na namna ya kuondokana na ukatili wa kijinsia.

Kwa upande wake, mwezeshaji wa mafunzo hayo Amina Tou, amesema kuwa wana imani walimu wanaohudhuria mafunzo hayo wataweza kuwaelimisha wengine katika shule zao ambapo pia watahakikisha wanafunzi watakaopewa elimu hiyo itawasaidia.

Mafunzo hayo yameanza kufanyika leo katika halmashauri 13 ambazo ni Ilala, Temeke, Ngorongoro, Ifakara, Kasulu, Kisarawe, Kibondo, Ulanga, Morogoro Mjini, Malinyi, Sengerema, Bagamoyo na Mlimba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles