Temesa yawatoa hofu abiria Kivukoni

0
1010

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), umetoa ufafanuzi na kukiri kuhusu hitilafu iliyosababisha wanaotumia magari kutopita kwenye kivuko (Ferry) kwenda na kurudi Kigamboni na kwamba hali ya usafiri imerejea kama kawaida.

Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano cha Wakala huo, leo Jumatano Desemba 9, imesema kuanzia saa 1:30 asubuhi kivuko cha MV. Magogoni kinachotoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni jijini Dar es Salaam kilipigwa na upepo mkali wakati kikikaribia upande wa Kigamboni.

“Hivyo, katika hali ya kupambana na upepo mitambo ya kuendeshea kivuko hicho iliingiliwa na takataka ambazo zilisababisha injini kupata moto na kupata hitilafu. “Mafundi wetu wamefanikiwa kutatua hitilafu hiyo na huduma za kivuko hicho zimerejea katika hali ya kawaida mnamo saa 6:30 mchana,” imesema taarifa hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here