24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

TEMDO yaanza kusaka mwarobaini wa vifaa tiba

Na Safina Sarwatt, Arusha

Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo ya Temdo Tanzania (TEMDO) imeanza kukabiliana na changamoto za vifaa tiba katika hospitali pamoja na vituo vya afya hapa nchini.

Kufuatia changamoto hizo TEMDO imefanya tafiti mbalimbali kwa lengo la kutatua nakuleta mabadiliko.

Akizungumza jijini Arusha katika Mkutano Mkuu wa 37 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), Mkurugenzi wa TEMDO, Mhandisi Prof. Frederick Kahimba amesema taasisi hiyo inamalengo makuu matatu ikiwemo kufanyatafiti zitakazo toa changamoto kwenye jamii, tunafanya huduma viwandani pale ambapo kunachangamoto.

“Kufanya mafunzo ya kihandisi kwa watu ambao wanafanya kazi ndani ya viwanda kwa ajili ya uendeshwaji, usalama viwandani pamoja mambo mbalimbali yanayohusiana na uzalishaji,” amesema Prof. Kahimba.

Amesema TEMDO inategeneza vifaa tiba kwa ajili hospitali zetu hapa nchini lengo nikupunguze uingizwaji wa vifaa kutoka nje ya nchi pamoja nakupunguza matumizi ya fedha za kigeni.

“Leo tumekuja kuonyesha vifaa tiba ambayo inatengenezwa TEMDO pamoja nakutoa elimu kwa Wajumbe wa mkutano mkuu wa 37 wa jumuiya ya tawala za mitaa Tanzania ALAT kwani wao ndiyo wasimamizi wakuu wa hospitali na viwanda hivyo tunamani kwamba hawataagiza vifaa tiba kutoka nje ya nchi tena,” amesema Prof. Kahimba.

Mkurugenzi wa TEMDO, Mhandisi Prof. Frederick Kahimba.

Amesema tayari taasisi hiyo imeweka mikakati mbalimbali kuhakikisha kuwa inazalisha vifaa vya kutosha.

Amesema vifaa hivyo ni pamoja vitanda vya wodi ya wajawazito, stendi za kuwekea drip, vitanda vya wagonjwa kufanyiwa uchunguzi pamoja na vitanda vya wagonjwa wanaolazwa hospitalini.

Amesema karakana hiyo kwa sasa inauwezo wa kutengeneza vitanda zaidi ya 500 vya wajawazito na vitanda na vya wagonjwa wanaolazwa hospitali.

“Taasisi yetu pia tunazalisha majokovu ya kuhifadhia maiti, pia tunategeneza viteketeza taka za mahospitali, hivyo tunakaribisha wadau wa afya na wamiliki wa hospitali binafsi na Serikali kununua vifaa tiba katika taasisi hiyo,” amesema .

Amesema TEMDO wametengeneza mashine za aina mbalimbali za kilimo, viwandani pamoja na kutoa elimu kwa wahandisi na mafundi uchundo nchini.

Amesema katika kipindi cha mwaka 2021/2022 taasisi hiyo iliwekeza zaidi ya Sh bilion 3 kwa ajili karakana ya kisasa ya kutengeneza vifaa tiba aina 17 ambapo mpaka sasa vifaa tiba aina saba (7) vimeanza kuzalishwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles