24.8 C
Dar es Salaam
Thursday, September 21, 2023

Contact us: [email protected]

Tembo auwa wawili ajeruhi watano

Ramadhan Hassan,Dodoma

Mbunge wa Mbulu Vijijini ,Flatei Massay (CCM)ameomba mwongozo bungeni akitaka Serikali imepe majibu kuhusiana na   tembo ambao wameua watu wawili na kujeruhi watano katika Jimbo lake.

Akiomba mwongozo leo Mei 28 bungeni mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu,Massay amemesema kwamba Tembo wameua watu wawili na wanaendelea kufanya uharibifu katika Jimbo lake.

“ Mhehimiwa Mwenyekiti naomba mwongozo  jambo hili limekuwa hatari na tembo wanaendelea kufanya uharibifu na watu watano wapo Hospital wakiwa wamejeruhiwa.

“Mheshimiwa Mwenyekiti naomba Serikali inisaidie kule kwa sababu tembo ni hatari wameendelea kuua watu wengi Jimboni,”amesema

Akijibu,Mwenyekiti wa Bunge,Najma Giga amesema“Naamini Serikali wameishalisikia, kuhusiana na vitendo vinavyohusiana na jambo hilo naamini kwamba watalifuatilia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles