32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Tembo auwa Mzee wa Miaka 91 Serengeti

Na Malima Lubashi, Serengeti

MKAZI wa Kijiji cha Parknyigoti katika Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Gibore Kitui(91) ameuwawa na Tembo wakati akichunga ng’ombe wake jirani na Hifadhi ya Pori la Akiba la Ikorongo.

Kaimu Mganga Mkuu Hospitali ya Nyerere DDH, Dk. Edga Saulo amekiri kupokea mwili wa marehemu saa 8 mchana ukisubiri uchunguzi wa polisi huku ukiwa na majeraha sehemu za tumboni baada ya kuuawa na tembo.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Parknyigoti, Mtiro Kikora akithibitisha kutokea kifo hicho amesema kimetokea Agosti 2, 2022 saa 4 asubuhi wakati Mzee huyo akiwa na wenzake wanachunga ng’ombe jirani na mpaka wa pori la akiba la Ikorongo lenye vichaka.

Amesema wakati mzee huyo anaendelea kuchunga baadhi ya ng’ombe waelekea kwenye vichaka ndipo aliamua kwenda kuwarudisha, ghafla alikutana na tembo watatu wakiwa na mtoto na kuanza kumfuku za kwa kumchoma pembe lake tumboni na kutokea upande wa pili hadi kupelekea utumbo kutoka nje na kusababisha kifo chake pale pale.

Mwenyekiti huyo ameomba Serikali kusaidia kuweka waya ya kuzuia wanyama kuingia maeneo kijijini kwake kama ilivyo katika vijiji jirani ambapo waya huo umesaidia kupunguza matukio ya uvamizi wa wanyama kuharibu mazao ya wananchi mashambani pamoja na vifo.

Ofisa Wanyamapori Pori Wilaya ya Serengeti, John Londeyani naye amethibitisha kutokea kifo cha mzee huyo kuuawa na tembo wakati akiwa machungani na mifugo yake umbali wa kilometa moja kutoka hifa dhi hiyo amewataka wananchi kuchukua tahadhari wanapokuwa jirani na maeneo ya hifadhi kwani hivi sasa tembo wameongezeka na wanapokuwa na watoto wanakuwa wakali kwa binadamu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Longinus Tibishibwamu alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo alidai ajalipokea ofisini kwake kwani yupo safari lakini akatoa wito kwa wananchi wanaoishi jirani na hifadhi za taifa kuwa makini wasiwaingiliye wanyama na kuwabughudhi.

Aidha, Kamanda Tibishubwamu pia amewataka wananchi kuendelea kuzingatia sheria zinazowataka kufanya shughuli jirani na hifadhi kwa kuchukuwa umakini wa hali juu .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles