27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Tembe homoni ya Progesterone husaidia kutopoteza ujauzito

TATIZO la wajawazito kupata hedhi limezidi kushamiri duniani kote.

Wapo ambao wamewahi kupoteza ujauzito au waliovuja damu bila kupoteza watoto katika miezi ya awali ni wengi mno.

Hata hivyo suala hili linahusishwa na matatizo ya kizazi au homoni.

Iwapo tatizo hilo linapatiwa tiba, basi upo uwezekano wa kujifungua salama, ambapo watafiti wanasema iwapo wajawazito wa aina hiyo watapewa homoni ya progesterone, tatizo huisha kabisa.

Watafiti nchini Uingereza walifanya majaribio hayo kwa wanawake 4000 waliokuwa na ujauzito.

Samantha Allen (31), ni miongoni mwa kina mama waliowahi kupata tatizo hilo wakati wa ujauzito.

Akiwa na ujauzito wa kwanza, Samantha alikuwa akivuja damu hadi akafikia hatua ya kumpoteza mwanawe, na tatizo hilo lilimkuta pia akiwa na mjamzito kwa mara ya pili.

Baada ya kupewa homoni Progesterone tatizo hilo liliisha na akafanikiwa kujifungua salama mtoto wa kiume aliyempa jina la Noah.

Wataalamu wanasema Progesterone ni homoni muhimu kwa wajawazito ambapo kazi yake kuu ni kuimarisha uzio wa kizazi sehemu ambako kijusi kinajiambatanisha na kusaidia mfumo wa kinga mwilini.

Samantha alipewa tembe za homoni ya Progesterone kwa majaribio, ambazo alizitumia mara mbili kwa siku hadi pale ujauzito wake ulipotimiza wiki 16.

Anasema aliacha kuvuja damu wiki moja tangu aaanze kutumia tembe hizo na aliendelea vizuri na ujauzito wake.

“Nadhani wanawake ambao waliwahi kuwa na tatizo kama langu sasa watanufaika. Hawatateseka tena kwani tatizo hili huathiri sana kisaikolojia,” anasema.

Takwimu zinaonesha kuwa mwanamke mmoja kati ya watano hupoteza ujauzito na mara nyingi uvujaji damu unahusishwa katika kuongeza hatari hiyo.

Samantha anasema: “Ninafurahi, siwezi kupata hatari yoyote kwa sababu yale hayakuwa majaribio ya kiwango cha awali.”

Utafiti huo wa Chuo Kikuu cha Birminghamuliochapishwa katika Jarida la Afya la New England, ulihusisha kundi la wajawazito 200 waliopewa homoni ya progesterone, huku kundi jingine la wanawake kama hao wakipewa tembe bandia.

Wote hao walikuwa wanavuja damu katika miezi ya kwanza ya ujauzito.

Licha ya kwamba utafiti huo umeonyesha si wanawake wote wanaovuja damu katika siku za kwanza wanaweza kusaidiwa kwa kutumia homoni hiyo, manufaa hayo ni makubwa miongoni mwa wanawake walio na historia ya kupoteza ujauzito (watoto watatu au zaidi).

Miongoni mwa wanawake hao, kulikuwa na ongezeko la asilimia 15 la waliojifungua, ambapo 98 kati ya 137 walifanikiwa kujifungua salama, wakati wale waliopewa tembe bandia 85 kati ya 148 ndio walijifungua.

Daktari wa Uzazi katika Hospitali ya Kina mama na Watoto Birmingham, Arri Coomarasamy, anasema matibabu hayo huenda yakasaidia kuokoa maisha ya maelfu ya watoto.

Anasema hata hivyo, matibabu hayo hayatofanya kazi kwa wanawake wote wanaopoteza ujauzito, kwa sababu kuna vyanzo vingi vya mimba hutoka.

Anasema wanaoweza kufaidika ni wale wenye tatizo la upungufu wa homoni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles