27 C
Dar es Salaam
Friday, May 27, 2022

Televisheni ya Citizen Kenya yajuta kumuita Rais Magufuli ‘mkaidi’

 NAIROBI, KENYA 

KITUO cha televisheni cha Citizen nchini Kenya chenye watazamaji wengi kimesema kinajuta kumuita rais Magufuli ‘mkaidi’.

Kituo hicho kilimuita Rais Magufuli hivyo katika taarifa yake ya habari iliyokuwa inahusu sera zake katika kukabiliana na mlipuko wa virusi vya corona.

Tanzania haijaweka masharti makali kuhusu mikutano ya watu kama ilivyofanywa na mataifa mengine duniani.

Katika ripoti hiyo ya Citizen iliopeperushwa hewani Machi 22, Rais Magufuli alinukuliwa akisema kwamba mlipuko wa virusi vya Covid-19 haufai kutumiwa kama sababu ya kuathiri uchumi wa Tanzania.

Kituo hicho kinachopeperusha matangazo yake katika eneo la Afrika Mashariki , kilisema katika ripoti hiyo kwamba haikuwa na madhumuni ya kuwapotosha raia wa Tanzania.

Taarifa hiyo ilisema :

“Tunanukuu: Tarehe 22 Machi , tuliripoti kuhusu mipango iliyowekwa na serikali ya Tanzania kukabiliana na janga la virusi vya corona. Katika ripoti hiyo tulimuita rais Magufuli ‘mkaidi’.

Tunanukuu ujumbe: Katika mahojiano na runinga ya Citizen , balozi wa Tanzania nchini Kenya alisema kwamba Magufuli anaunga mkono juhudi za kieneo na kimataifa kukabiliana na mlipuko wa virusi vya corona .

Tunanukuu ujumbe: matumizi ya neno ‘mkaidi’ dhidi ya rais Magufuli hayana msingi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,454FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles