24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

TEKNOLOJIA ZILIZOKUFA 2016

Na FARAJA MASINDE


 

MWAKA 2016 umefika ukingoni, unatupa mkono wa kwa heri kwani umebakiza saa 24 kabla ya kuingia 2017. Ahsante kwa wewe ambaye umekuwa mfuatiliaji wa safu hii.

Ni wazi kuwa kwa mwaka huu kuna mambo mengi ambayo yamefanyika, ikiwamo teknolojia ya ndege za Drones kwa ajili ya kamera, ni wazi kuwa ulikuwa ni mwaka mzuri kwa kampuni nyingi za teknolojia.

Bidhaa mbalimbali, pia zipo teknolojia zilizofanikiwa na kufa pia ndani ya kipindi hiki cha miezi 12. Hizi ni kati ya zilizokufa 2016.

iPhone yaachana na ‘headphone jack’

Septemba mwaka huu kwa mara ya kwanza kampuni ya utengenezaji simu za iPhone ya Apple imeachana na headphone zilizozoeleka kutumiwa na kampuni hiyo za ‘jack’ na kutambulisha headphone mpya ambazo hazitumii waya za ‘AirPods’, zilizoenda sambamba na uzinduzi wa simu yake mpya ya iPhone 7.

Licha ya kwamba itachukua muda kwa wateja kuzizoea lakini hiyo ni moja ya kampeni ya Apple ya kuhakikisha kuwa wanawekeza nguvu kubwa kwenye soko la sauti.

 

Samsung Galaxy Note 7

Mwaka huu utasalia kuwa pigo kwa kampuni hii ya Kikorea kwani tumeshuhudia ikikumbana na wakati mgumu kwenye simu zake za Galaxy Note 7, ambapo Oktoba mwaka huu kampuni hiyo iliamua kuagiza kurejeshwa sokoni kwa simu hizo zote kufuatia kuwapo kwa malalamiko kila kona ya dunia kutoka kwa wateja juu ya kulipuka kwa simu hizo.

Kwasasa huwezi kupanda ndege iwapo utakuwa na simu ya Note 7 jambo ambalo limetia doa brand ya kampuni hii.

Kufa kwa simu za BlackBerry

Pia tumeshuhudia kampuni ya BlackBerry iliyokuwa ikijulikana kwa kutengeneza simu zinazotumia batani, ikiachana kabisa na utengenezaji wa simu.

BlackBerry ilitangaza ifikapo Septemba kuwa ingeachana na utengenezaji simu na kujikita kwenye kuendeleza Software zake, kampuni hiyo imekuwa na wakati mgumu sokoni kwa kipindi kirefu.

Kabla ya kuja kwa simu za iPhone, simu za kampuni hiyo zilikuwa zikipendwa zaidi duniani ambapo Rais Barack Obama wa Marekani alikuwa ni miongoni mwa watumiaji.

Motorola

Pia kumeshuhudiwa kampuni ya Lenovo ikiiua ile ya Motorola mapema mwaka huu, badala yake kwasasa kampuni hizo zinajulikana kama “Moto by Lenovo”.

VCRs

Kampuni hii kutoka Japani ilikuwa ikijulikana kwa kutengeneza deki za mikanda ya video tangu 1960, hata hivyo mwaka huu imefungwa baada ya kukabiliwa na ushindani mkali wa soko kutoka kwenye deki za CD kwa maana ya, DVD na Blu-ray.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles