30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

TEKNOLOJIA YA ROBOTI HATARINI KUPIGWA MARUFUKU

Na FARAJA MASINDE


SAFU hii iliwahi kuzungumzia juu ya mapinduzi makubwa ya teknolojia ya roboti duniani ambayo yataenda sambamba na na kasi ya 5G.

Ukuaji wa teknolojia hii ni kwamba unatishia nguvu kazi ya binadamu ikiwa na maana kuwa kazi nyingi zinazofanywa na binadamu kwa sasa zitakuwa zikifanywa na roboti.

Hatari hii ndiyo imefanya Umoja wa Ulaya (EU) kushindwa kujizuia ambapo tayari umetangaza kuwasilisha muswada wa kudhibiti matumizi ya teknolojia ya roboti.

Mbali na kudhibiti matumizi hayo ambayo yanatishia vibarua vya watu, pia muswada huo unapendekeza roboti hizo kutozwa ushuru wa kodi.

Muswada huo umewasilishwa na Bunge la Umoja wa Ulaya kupitia kamati ya Mambo ya Ndani.

“Kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo na idadi ya roboti inavyozidi kuongezeka kwenye maisha yetu ya kila siku, jambo ambalo linaelekea kuathiri maisha  ya watu kwa ujumla.

“Kwani Roboti hizi zinaelekea hadi kuanza kuandaa mkate jambo ambalo ni hatari mno,” anasema Mady Delvaux ambaye alikuwa ni mwasilishaji wa mswada huo.

Musawada huo unataka kuwekwa kwa utambulisho maalumu ambao itakuwa unatoa maelekezo kwa wahandisi wanaotayarisha roboti hizo kutengeneza kwa kuzingatia maadili na usalama wa bidhaa hiyo.

Moja kati ya masharti hayo ni kuhakikisha kuwa roboti hizo zinawekewa kifaa maalumu kitakachokuwa tayari kuizima mara moja pindi inapotokea dharura tofauti na sasa.

EU pia imewaagiza watengenezaji hao kuhakikisha kuwa teknolojia ya roboti hizo zinaweza kubadilishwa iwapo zitashindwa kufanya kazi kama ilivyokusudiwa.

Jambo jingine kwenye mswada huo ni kuhakikisha kuwa roboti hizo haziui mtu yeyote na kwamba wakati wote zitakuwa zikiongozwa na binadamu na si vinginevyo, huku pia zikitakiwa kufanya kazi kwa kiasi ili kuokoa ajira za watu.

“Nilazima watengenezaji wajue kuwa roboti si binadamu na kamwe haziwezi kuwa, wala kuwa na upendo kwa binadamu,” anasema Delvaux.

Pia muswaada huo unataka kuwapo na bima kwenye roboti hizo ili kuweza kulipa fidia iwapo itatokea zimeleta madhahara kwa binadamu au kufanya kazi kinyume na utaratibu.

Jambo jingine ni kuhakikisha kuwa zinalipa kodi iwapo matumiizi yake yatakuwa makubwa kushinda binadamu.

EU imesema kuwa ni lazima roboti hizo zote zilipiwe kodi hiyo kama ambavyo binadamu wamekuwa wakifanya lengo likiwa ni kuendelea kukusanya mapato ya kutosha kama vile ambavyo imekuwa ikikusanya kwa binadamu.

Lengo la kuweka masharti hayo kwenye teknolojia hiyo inayotarajiwa kuchukua kazi za watu wengi duniani ni kuhakikisha kuwa inadhibiti matumizi hayo ili kulinda ajira za watu wengi barani humo na duniani kwa ujumla.

Je, unafikiri masharti haya yatarudisha nyuma teknolojia hii? Tusubiri tuone. 0653045474

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles