26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Teknolojia ya LoRa yatajwa kuwa nyenzo muhimu katika kulinda wanyama

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

Teknolojia ya kisasa ya LoRa inayotumika kufuatilia mienendo ya Wanyama adimu aina ya faru katika Hifadhi za Serengeti na Mkomazi, pamoja na “GPS collar” zinazotumika kufuatilia mbwa mwitu katika hifadhi ya serengeti na tembo katika Hifadhi ya Ruaha imeelezwa kuwa nyenzo muhimu katika kulinda wanyama.

Hayo yameelezwa na Ofisa Mhifadhi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA), July Lymo wakati akiwasilisha wasilisho kuhusu hifadhi za taifa  kwa  Waandishi wa Habari.

Mkutano huo ulikuwa na lengo la kuandaa mkakati wa kutangaza Utalii wa ndani, Tanapa kwa kushirikiana na waandishi wa habari wa mkoa wa Dodoma.

Mhifadhi huyo amesema mojawapo ya mafanikio ya Tanapa ni katika uhifadhi wa wanyama ambapo kwa sasa Teknolojia ya kisasa ya LoRa inayotumika kufuatilia mienendo ya Wanyama adimu aina ya faru katika hifadhi za serengeti na mkomazi, pamoja na “GPS collar” zinazotumika kufuatilia mbwa mwitu katika hifadhi ya serengeti na tembo katika Hifadhi ya Ruaha imesaidia kulinda wanyama.

Pia amesema wanyama aina ya pundamilia na swala wamehamishiwa (translocated) katika hifadhi za Kitulo na Saadani, pamoja na simba katika Hifadhi ya Kisiwa cha Saanane.

Kuhusiana na ulinzi wa rasilimali na wanyamapori,amesema matukio ya ujangili wa tembo yamepungua kwa takribani asilimia 99 na kwa kipindi cha miaka miwili (2019 – 2020) hakuna tukio la kuuawa kwa tembo lililothibitishwa ndani ya mipaka ya hifadhi za taifa.

Amesema hatua hiyo imekuja kufuatia (TANAPA) kuendelea kuboresha mbinu za ulinzi ili kudhibiti ujangili wa tembo na wanyama wengine ndani na pembezoni mwa hifadhi za taifa.

“Ulinzi wa rasilimali za taifa katika hifadhi na mapambano dhidi ya ujangili yanafanywa kwa mbinu za kisasa na weledi ikiwa ni pamoja na kufanya doria zinazo ongozwa na taarifa kiintelijensia na kutumia vifaa vya kisasa vya kielektroniki. kazi kwa urahisi na muda mfupi,”amesema.

Kwa upande wake, Kamishna Mhifadhi Msaidizi  Mwandamizi kutoka Kitengo cha Mawasilino Tanapa, Paschal Shelutete amesema moja ya mkakati walionayo ni pamoja na kuimarisha miundombinu ya utalii hususani barabara,viwanja vya ndege,malango,mawasiliano,maji na umeme ili kuzidi kuwavutia watalii wa ndani na nje  ya nchi.

Shelutete amesema Tanapa linafanya shughuli zake kulingana na mpango mkakati wa miaka mitano (2018/19-2022/23) ambao umefanyiwa marejeo na kuandaa mkakati mwingine wa miaka mitano (2021/22 –2025/26).

Shelutete amesema kipindi cha mvua hali huwa sio nzuri katika mbuga mbalimbali  hivyo,Tanapa imejipanga kuhakikisha maeneo hayo yanafikika ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya watalii.

Naye,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Dodoma, Ahmed Mbugi amewataka waandishi wa habari kupasa sauti kuhusiana na vivutio vya utalii  vilivyopo nchini huku akiwaomba wananchi kutembelea vivutio vya ndani kama ilivyo kwa nchi ya Afrika ya Kusini.

“Kwa hiyo ni vyema kushirkiana vizuri tunaweza kufika mahali, serikali mkazo sasa hivi ni kusaidia kutangaza watalii kuna Nchi wageni robo tatu wanatoka ndani ya nchi mfano ni Afrika Kusini ni moja ya nchi ambazo watalii wengi ni wakazi wa Afrika Kusini, kwenye mahifadhi yao mengi ukienda utakutana nao ukimuuliza anasema anatoka humo humo,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles