25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

TEKNOLOJIA HUTUMIWA NA VIKOSI HATARI ZAIDI DUNIANI

Na JUSTIN DAMIAN


 

UMOJA wa Kujihami wa Nchi za Ulaya Magharibi (NATO) linavielezea vikosi maalumu kama vikosi ambavyo hutumika kwenye operesheni maalumu na ngumu ambazo vikosi vya kawaida vya ulinzi na usalama haviwezi kufanya. Vikosi maalumu huundwa na watu wenye mafunzo ya hali ya juu na magumu huku wakitumia silaha pamoja na teknalojia za kisasa.

Kutegemeana na nchi husika, vikosi maalumu vinaweza kutumika kuokoa mateka, kupambana na magaidi, kuzuia mapinduzi ya kijeshi, operesheni za kiitelijensia pamoja na operesheni nyingine ngumu. Kwa msaada wa tovuti ya Defence Updates, safu hii itavimulika vikosi vitano ambavyo vinaamika kuwa  hatari zaidi duniani na ambavyo vinaweza kufanya operesheni ngumu

 

  1. MARCOS INDIA

Mafunzo magumu na ya hali ya juu yanafanya kikosi hiki cha India kuwa moja kati ya vikosi vyenye uwezo wa kufanya operesheni zenye utata na ngumu. Ushirikiano kati ya yake na kikosi cha Navy Seals cha Marekani ambacho pia tutakiangalia baadaye, kinakifanya kuwa na uwezo wa kufanya operesheni kwa kuwadondosha askari kutoka angani pasipo ufahamu wa adui. Kikosi hiki kinaweza kudondoshwa katikati ya bahari na kujipanga vizuri kisha kufanya operesheni isyo na makosa.

Askari wawili wa kikosi hiki wanao uwezo wa kulinda eneo lenye ukubwa wa kilomita za zaidi ya 250 la Ziwa Wular na kuzuia lisitumiwe na magaidi wanaotokea nchini Pakistan kuingia India. Kikosi hiki ndiyo ambacho kinaogopwa zaidi na magaidi ambao wamekuwa wakiweka kambi zao nchini Pakistan.

Silaha za kisasa ambazo wanazitumia ni pamoja na Pistol Auto 9mm 1A 9mm Semi-automatic pistol. Beretta 92FS Semi-automatic pistol, Sako Tikka T3 TAC 7.62x51mm na bolt-action sniper rifles.

Nyingine ni pamoja na SAF Carbine 2A1 9mm Sub-machine gun. Heckler & Koch MP5A3/A5 9mm Sub-machine gun. AK-103 7.62×39mm Assault rifle na  AKMS 7.62×39mm Assault rifle

 

Baadhi ya opereshi ngumu walizowahi kuzifanya

Mwaka 1988 kikosi kilifanikiwa kuzima jaribio la kuiangusha Serikali Kisiwa cha Maldive. Kilikamata boti iliyokuwa na wanajeshi 46 wenye silaha pamoja na mateka ambao walikuwa wakijaribu kutoroshwa baada ya kushindwa kutekeleza jaribio hilo.

Mwaka 2008 wakati wa shambulio la kigaidi katika mji wa Mumbai nchini India waliweza kuingia katika hoteli ya Taj na kuwanasa magaidi waliokuwa wamejificha ndani ya hoteli hiyo.

 

  1. SPETSGRUPPA ‘A’ LA URUSI

Kikosi hiki pia huitwa Alpha Group kikiwa ni sehemu ya jeshi la ulinzi la Urusi. Kinaweza kufanya operesheni tata pasipo kutegemea msaada wowote huku kikitumia askari wachache ambao hutumia teknalojia na mafunzo ya hali ya juu. Kiliundwa kwa mara ya kwanza mwaka 1974 na Shirika la Ujasusi (KGB) la wakati huo iliyokuwa Jamuhuri ya Kisovieti

Japokuwa haifahamiki vizuri kuhusiana na majukumu yake pamoja na operesheni ambazo inafanya, inaaminika kuwa kinafanya kazi kwa kupokea maelekezo kutoka kwa uongozi wa juu wa kisiasa wa nchi hiyo.

Mwaka 1985 wanadiplomasia wanne wa nchi hiyo walikamatwa na kundi la Waislamu wenye msimamo mkali lililokuwa linajiita Islamic Liberation Organisation katika mji wa Beirut nchini Lebanon. Urusi ililituma kundi Alpha Group na lilifanikiwa kumkamata kiongozi mkuu wa watekaji pamoja na ndugu za watekaji wengine. Alpha group walimuasi kiongozi huyo na kumkata vipande vipande na kisha kupeleka vipande vyake kwa watekaji nyara.

 

Walitishia kuwaua ndugu wa watekaji nyara hao endapo wasipowaachia wanadiplomasia wa Urusi. Matokeo yake ni kwamba wanadiplamasia waliokuwa wametekwa waliachiliwa na hakuna afisa yeyote wa Urusi aliyetekwa tena pamoja na wimbi kubwa la utekaji nyara lililokuwa linaendeshwa na kundi hilo katika eneo la Mashariki ya kati.

Wiki ijayo tutaangalia vikosi viwili hatari kuliko vingine duniani ambavyo ni Seal cha Marekani na SAS cha Uingereza.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles