26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

TEKNO APATA MTOTO WA KWANZA

LAGOS, NIGERIA


STAA aliyetamba na wimbo wa ‘Pana’, Augustine Kelechi maarufu kwa jina la Tekno Miles, amethibitisha kupata mtoto wa kwanza na mpenzi wake, Lola Rae.

Hata hivyo, Tekno na mrembo huyo walitangaza kuachana miezi sita iliyopita wakati huo Lola akiwa mjamzito, kila mmoja alimwondoa mwenzake kwenye akaunti ya Instagram, lakini kupitia ukurasa huo wa Tekno ameweka wazi kuwa amepata mtoto.

Inasemekana wawili hao walimaliza tofauti zao mapema kabla ya mrembo huyo kujifungua mwishoni mwa wiki iliyopita.

“Hatimaye tumefikia kilele, nina furaha kubwa kupata mtoto,” aliandika Tekno kwenye ukurasa wake wa Instagram, akiambatanisha na alama nyingi zenye upendo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles