23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

TEF yatuma salamu za rambirambi vifo vya wafanyakazi wa Azam

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Jukwaa la  Wahariri Tanzania (TEF), limetuma salamu za rambirambi kutokana na vifo vya watu saba wakiwamo wafanyakazi watano wa Azam Media waliofariki katika ajali ya gari iliyotokea kati ya Shelui na Igunga.

Ajali hiyo imetokea leo Jumatatu Julai 8 asubuhi, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana na lori wakati wafanyakazi hao wakiwa njiani kuelekea Chato kwa ajili ya kwenda kuonesha matangazo ya moja kwa moja ya uzinduzi wa Hifadhi ya Burigi kesho Jumanne Julai 9.

Kwa mujibu wa wa taarifa iliyotolewa na TEF leo imeelezea masikitiko yao baada ya vifo vya wafanyakazi wa Azam Media  waliokuwa safarini kwenda Chato kutekeleza wajibu wao wa kitaaluma.

“Tunaungana na wanataaluma wote wa tasnia ya habari nchini kuupa pole uongozi na wafanyakazi wote wa Azam Media, kutokana na pigo kubwa la kupoteza wafanyakazi wake watano kwa mpigo, hakika ajali hii imeacha simanzi kubwa kwa tasnia ya habari na wanahabari kwa ujumla.

“Hili ni pigo kubwa kwa taaluma ya habari nchini, TEF tumehuzunishwa, kusikitishwa na kuumizwa na msiba huu kwani tasnia imewapoteza wafanyakazi wanataaluma mahiri ambao walikuwa wakielekea Chato mkoani Geita, kutekeleza wajibu wao wa kitaaluma wa kuwafahamisha Watanzania na dunia kwa ujumla tukio la uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi,  Chato,” imesema taarifa hiyo.

Aidha mbali na wafanyakazi hao wa Azam, ajali pia hiyo imesababisha vifo vya dereva wa gari la kukodi aina ya ‘Coaster’ na msaidizi wake huku wafanyakazi wengine watatu wa Azam wakijeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya Wilaya Igunga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles