23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

TEF yamuonya Haji Manara udhalilishaji kwa Waandishi wa Habari

Na Brighter Masaki, Mtanzania Digital

Siku mbili baada kufanyika Mkutano wa Klabu ya Simba na Waandishi wa habari, ambapo Msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara alionyesha kumdhalilisha Mwanahabari wa Clouds FM, Prisca Kishamba, Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limesikitika na kulaani kitendo hicho.

Jukwaa la wahariri linalaani kitendo cha msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara kumdhalilisha mwandishi wa Habari Prisca Kishamba.

Taarifa iliyotolewa na jukwaa hilo leo Ijumaa Julai 2, 2021 na Mwenyekiti wake, Deodatus Balile imeeleza kuwa udhalilishaji huo ulioambatana na maneno ya kashfa ulifanywa kwenye mkutano wa Simba na waandishi wa habari uliofanyika Juni 30, 2021 mkoani Dar es Salaam.

TEF imemtaka Manara kuacha mara moja tabia ya kutumia mikutano ya klabu ya Simba na hata mitandao ya kijamii kuwadhalilisha Wanahabari.

Limesema ikiwa kuna suala lolote ambalo mwandishi wa habari amelitenda kinyume cha maadili na miongozo ya taaluma, wahusika wanapaswa kuwasilisha malalamiko yao kwa taasisi za kihabari au kwa mwajiri wa mwandishi husika ili hatua ziweze kuchukuliwa.

Kupitia taarifa hiyo, TEF imeuomba uongozi wa timu hiyo inayoongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kumuonya Manara kuacha tabia hizo mara moja kwani hazina afya na haziongezi thamani yoyote kwa Simba wala taaluma ya habari.

“Ikiwa vitendo vya aina hii vitaendelea kujitokeza, TEF kwa kushirikiana na taasisi nyingine za kihabari na vyombo vya habari hatutakuwa na njia nyingine zaidi ya kuchukua hatua zaidi Ili kuwaepusha waandishi wetu dhidi ya unyanyaswaji na udhalilishwaji,” amesema Balile.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles