30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

TEC yasema ni Katiba ya CCM

Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Askofu Severin Niwemugizi
Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Askofu Severin Niwemugizi

NORA DAMIANI, DAR ES SALAAM

MAKAMU wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa Katoliki (TEC), Askofu Severin Niwemugizi, amesema licha ya Rasimu ya Katiba inayopendekezwa kupitishwa na wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba jana, kelele za kudai Katiba Mpya hazitaisha kwani mchakato wa upatikanaji wake haukuwa wa maridhiano.

Akizungumza na gazeti hili jana, Askofu Niwemugizi alisema mchakato mzima umeendeshwa kwa mtazamo, matakwa na mapenzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alisema kwa maana hiyo, kelele za Katiba Mpya zitaendelea na kutahadharisha kuwa hali hiyo ni hatari kwa usalama wa nchi.

“Sichukii chama chochote na wala mimi si mwanachama wa chama chochote, lakini naona mambo yalivyofanyika si sawa,” alisema.

Askofu huyo ambaye huwa na msimamo usiotetereka, alisema tangu mwanzo zilifanyika mbinu ili rasimu hiyo ipitishwe, lakini wananchi ndio watakuwa waamuzi wa mwisho.

“Wananchi wenyewe ndio watakuwa waamuzi wa mwisho, hatupaswi kuwa na magomvi yoyote, wananchi wana mamlaka ya kuamua kama wanaitaka hii Katiba au la,” alisema.

Hata hivyo, askofu huyo alisema anaamini viongozi wa Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF) watakutana kuzungumza na kushauri cha kufanya.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Ushindi was hila, fitina, mabavu, vitisho na mbinu za kishetani siyo ushindi. Huko ni kushindwa. Lazima ujue kwamba “Uwongo na uovu hauwezi kushindwa hats shikumoja baliukweli” Inafahamika wazi kwamba katiba ni safai ndefu kule kenya ilichukua miaka zaidi ya 20, sasa hii ni kawaida chama twala kutumia mabavu, lakini itafika wakati wananchi wenyewe watatambua na kusema , hapana. Mimi ninaamini watanzania wa leo si wa jana, hivi kusherekea ushindi wa hila siyo hoja. Kilichopitishwa si katiba ni rasimu, katiba itapitishwa na wananchi katika kura za maoni. Ninaamini kama Watanzania wanaipenda nchi yao basi ni lazima waungane kuachana na katiba hii yakiharamia, ambayo haitawasaidia. Hata wale wanaoishabiki, ni kwa ababu hawaelwi maana ya katibna ya nchi. Hivi basi mimi naungana na Askofu Niwemugizi kwamba, watanzania wataamua wakiataka katiba mabaya sawa, na wakitaka katiba nzuri mchakato utarudiwa, siyo kitu cha ajabu kurudia mchakato mzima kama kuna kssoro. Mimi naamini katiba hii haitafika pipote, ni ushindi wa leo tu na kujiridhisha nafsi, ingawaje CCM wenyewe wanajua walichofanya ni uchakachuaji na uharamia. “Sauti ya wengi anayoongelea pinda ni ipi? Uwingi wa CCM bungeni, hapana, sauri ya wengi ni wananchi maskini, hyuwezi kukusnya marafiki wa dunia nzima wakafanya maamuzi yakipuuzi halafu unaita ndiyo sauti ya wengi, huku ni kupotosha maana ya sauti ya wengi, ndiyo sauti ya Mungu. CCM mtajaribu kuhalalisha uovu wetu hata kumwita Mungu aliyembinguni na malaika wote, utabaki ni uovu tu. Mimi nahesabu wananchi mmeshinda katika hili. Kazi ya kanisa ni kutafuta masilahi ya taifa , ya wananchi, hivi naungana na viongozi wa Jukwaa la Kikristo kwamba wanendelee kukutana na kuinusuu nchi hii kutoka katika mikonoyakatiba hii a kikandamizaji. Wananchi mjue kama mtaipitisha, basi mjue mchi hii itakuwa mabaya kulikonchi ziote zinazotawaliwa kidikiteta (Iran, Iraq, Somalia, na kwingineko). lakini mimi naamini kwamba Mungu yupo upande wa Wananchi, na wanachi daima watashinda hata kama siyo leo. Wapinzani lazima waendelee kuleimisha wananchi juu ya uchakachuaji huo ili waweze kupiga kura yao vema. Na tusipoangalia uchaguzi wa mwakanai unaweza kuwa ndiyo chanzo cha machafuko kama ilivyokea Kenya, kwani uchagui lazima uandaliwe vema, lakini inachoonekana sasa CCM wanataka kulazimisha katiba ipite kabla ya uchaguzi, ili waendelee kutumia katiba mbovu, watanzania ni vema tukakataa sula la kukimbiza katiba kuna nini, wakati vyama vya kisiasa vilikubaliana na Rais, au tuseme hiyo ilikuwa nimbinu ya kuwalainisha wapinzani ili mchakato uendelee. Wapinzani lazima sasa muangalie maafikiano mnayofanya na viongoxi wa serikali, kwani huwa hamjui agenda zao za siri, ni afadhali kuweka msimamo wa pamoja na kuufuata kikamilifu. MUngu wabariki watanzania wanaolilia katiba mpya bado.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles