29.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

TDCD yabainisha mwelekeo wake kuimarisha Ushirika 2023/24

Mwandishi Wetu,Mtanzania Digital

TUME ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TDCD) imetaja mwelekeo wake katika kuimarisha ushirika kwa mwaka 2023-2024 ikiwemo kuharakisha mchakato wa uanzishwaji wa Benki ya Taifa ya Ushirika ili kuviwezesha Vyama vya Ushirika kupata mikopo yenye riba nafuu.

Hayo yameelezwa leo Ijumaa, Agosti 11,2023 jijini Dodoma na Mtendaji Mkuu wa (TCDC), Dk. Benson Ndiege wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji na vipaumbele vya Tume hiyo kwa mwaka 2023-2024.

Mkurugenzi huyo amesema hadi kufikia Desemba 2024, Tume itakuwa imeshazindua Benki ya Taifa ya Ushirika (KCBL).

“Na kuwa mali ya wanachama katika kujipatia mikopo ya kuendesha shughuli zao kikamilifu,” amesema Dk. Ndiege.

Ameutaja mwelekeo mwingine ni uwekezaji katika mifumo ya kisasa ya kidijitali ili kuongeza ufanisi wa kiutendaji katika Vyama vya Ushirika, pamoja na Mamlaka za Usimamizi.

“Kuhamasisha mfumo wa Ushirika, kujiendesha kibiashara wenye kuaminika na shindani ukijikita kwenye kuongeza thamani ya uzalishaji katika Vyama,” amesema Dk. Ndiege.

Pia, kuboresha sera, sheria na usimamizi wa Ushirika ili kuchochea ukuaji na maendeleo ya Ushirika imara Tanzania.

Vilevile, kuhamasisha Ushirika kwenye sekta mbalimbali na makundi maalum ili kuhakikisha wananchi wengi zaidi wananufaika na mfumo wa ushirika.

Pia, kuimarisha uwekezaji wa mali za ushirika katika uzalishaji.

Amesema mwelekeo mwingine ni kushirikiana na wadau mbalimbali katika kutatua changamoto zilizopo kwenye ushirika.

Mkurugenzi huyo amesema hadi kufiki Machi 2023, Tume ilinunua kompyuta 226, viti 70, magari 12 na pikipiki 147.

Pia, imepokea magari matatu kutoka Wizara ya Fedha na gari moja kutoka Taasisi isiyo ya Kiserikali (Heifer International) kwa ajili ya Ofisi za mikoa.

Amesema hadi kufikia Juni, 2023, vyama vya Ushirika 5,424 kati 7,300 vimesajiliwa katika Mfumo huo, unaolenga kurahisisha usimamizi na uendeshaji wa Vyama vya Ushirika kwa nia ya kuongeza ufanisi, uwazi na uwajibikaji.

Amesema mafunzo kwa watekelezaji wa Sheria 62 yametolewa Mikoa ya Tanzania Bara ili kupunguza migogoro kwenye Vyama na kuondoa dosari katika utendaji wa vyama vya ushirika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles