26.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

TCU yasitisha udahili vyuo vilivyofungiwa

Asha Bani, Dar es Salaam

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), imesitisha udahili wa wanafunzi wapya wa ngazi zote za masomo katika vyuo vikuu mbalimbali nchini ambavyo vilifungiwa.

Vyuo hivyo ni vile vilivyofungiwa mwaka 2017 na kutakiwa kufanya maboresho mbalimbali yakiwamo ya kujifunzia na kufundishia lakini hawakufanikiwa kurekebisha dosari hizo.

Kwa mujibu Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa vyuo hivyo ni Chuo Kikuu Kishiriki cha Josiah Kibira (JOKUCo), Chuo Kikuu cha Mlima Meru (MMU), Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolohoa (IMTU) na Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UoB).

Vingine ni Chuo Kikuu Kishiriki cha Uhandisi na Teknolojia cha Mt. Yosefu (SJUCET), Chuo Kikuu Kishiriki cha Kikristo cha Tiba Kilimanjaro (KCMUCo) na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Stefano Moshi (SMMUCo).

“Itakumbukwa kwamba kati ya Oktoba 2016 na Januari 2017, TCU ilifanya ukaguzi maalumu wa kitaaluma kwa taasisi zote 64 za vyuo.vikuu vishiriki na vituo vya vyuo vikuu.

“Lengo lilikuwa kuhakikisha kuwa elimu ya juu itolewayo inakidhi viwango vya ubora kitaifa, kikanda na kimataifa ambapo matokeo ya ukaguzi yalibainisha kasoro mbalimbali katika uendeshaji wa vyuo vikuu nchini,” amesema Profesa Kihampa.

Pamoja na mambo mengine, amesema vyuo vikuu 19 vilikutwa na kasoro kubwa na kwamba vilipewa ushauri na muda wa marekebisho hata hivyo havikuweza kufanya marekebisho hayo katika kipindi kifupi na kuzuiliwa udahili kwa mwaka 2017 na 2018.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles