TCU YAFUTA UDAHILI KWA VYUO 19 NCHINI

1
1065

Tume ya Vyuo vikuu (TCU) imevifutia udahili vyuo 19 na kufuta kozi 75 katika vyuo  22 kwa kukiuka Sheria taratibu na kanuni za utoaji wa elimu ya juu hapa nchini.

Ofisa Habari wa Tume hiyo Edward Mkaku amesema uamuzi wa kuvifutia udahili baadhi ya vyuo ni kutekeleza agizo la serikali lililoitaka Tume hiyo kuvisimamia kwa karibu vyuo ili viweze kutoa elimu bora.

Makaku amesema kwa vyuo ambavyo wanafunzi wanaendelea na masomo mabadiliko haya hayatawahusu wanatakiwa kuendelea na masomo kama kawaida, isipokuwa vyuo hivyo  havitaruhusiwa kudahili wanafunzi wapya kwa mwaka huu wa masomo.

Aidha, amesema baadhi ya sababu za vyuo hivyo kufutiwa udahili wa Shahada, Shahada za Uzamili pamoja na Shahada za Uzamivu kuwa ni kukosa vitendeakazi na wataalamu katika kufundisha elimu ya juu.

Alivitaja baadhi ya vyuo vinavyotoa taaluma za afya kama Kilimanjaro Christian Medical College (KCMC) cha mkoani Kilimanjaro, Kampala International University (KIU) na  Hubert Kairuki Memorial University (HKMU) vya Jijini  Dar es Salaam ambavyo vilikuwa vikitoa kozi za udaktari, ufamasia pamoja na shahada ya uzamili katika Udaktari wa magonjwa ya wanawake iliyokuwa ikitolewa na Chuo cha Hubert Kairuki  imebainika kuwa hawakuwa na vifaa na wataalamu wa kutosha kufundisha kozi hizo.

Vyuo vingine ni St. Joseph, St. John, Tumaini University pamoja na vyuo vingine kadhaa ambavyo havina waalimu pamoja na vifaa kwa mujibu wa maelekezo ya Tume hiyo.

 

 

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here