24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

TCU yafungua dirisha la usajili elimu ya juu

Na TUNU NASSOR, DAR ES SALAAM

TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), imefungua dirisha la kwanza la maombi ya usajili kwa shahada ya kwanza ili kutoa nafasi kwa wanafunzi wengi kutuma maombi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa alisema,  dirisha hilo lililofunguliwa rasmi kuanzia jana litafungwa rasmi Septemba 25, mwaka huu.

Alisema waombaji wanahimizwa kupata taarifa rasmi kupitia tovuti ya TCU na vyuo vilivyo ruhusiwa kudahili wanafunzi wa shahada za kwanza na taarifa zinazotolewa na TCU kupitia vyombo vya habari.

“TCU inampenda.kuutarifu umma, taasisi za elimu ya kuu ndani na nje ya nchi kuwa, kufuatia kutangaza kwa matokeo ya kidato cha sita imefungua dirisha la kwanza la.maombi ya shahada ya kwanza kuanzia leo badala ya Agosti 31, mwaka huu iliyopangwa awali,” alisema Kihampa.

Kihampa alisema ili.kufahamu sifa stahili kwa waombaji watatakiwa kusoma vigezo vilivyooonyeshwa katika kitabu Cha miongozo ya TCU ambacho KIPP katika tovuti hao.

Aliwataka waombaji kuwa makini kabla ya kutuma maombi kwa kusoma miongozo iliyotolewa.

Alisisitiza kuwa waombaji wenye vyeti vilivyotokea nje ya nchi ni lazima.wawasilishe vyeti vyao Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte), ili kupata ithibati ya ulinganifu wa sifa zao kabla ya kutuma maombi.

Profesa Kihampa, aliwataka wananchi kuepuka kupotoshwa na watu wanaojiita mawakalanau washauri wanadai wanatoa huduma jinsi ya kujikinga na vyuo hovyo hapa nchini.

Katika hatua nyingine, tume hiyo imetangaza maonyesho ya 15 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yatakayofanyika Agosti 31 hadi Septemba 5, mwaka juu jijiji Dar es Salaam.

Kihampa alisema maonyesho hayo yatatoa fursa kwa wadau wa elimu na wanafunzi kuonana ana kwa ana na vyuo vya elimu ya juu.

“Tume inawahimiza waombaji wa udahili, wawekezaji na wananchi kwa jumla kuhudhuria katika maonyesho hayo ili kupata fursa ya kuonana na vyuo husika,” alisema Profesa Kihampa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles