26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

TCU: Hatutoi tena mikopo mipya

Cosmas Mwaisobwa
Cosmas Mwaisobwa

Na LEONARD MANG’OHA, DAR ES SALAAM

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imesema haiwezi kutoa mikopo kwa waombaji wapya walioomba baada ya Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kushusha viwango vya udahili.

Wiki iliyopita, TCU ilitangaza kushusha viwango vya udahili bila kueleza sababu za kufanya hivyo.

Akizungumza na MTANZANIA, Dar es Salaam  jana, Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano, Cosmas Mwaisobwa, alisema tume  hiyo haiwezi kuongeza muda kwa wanafunzi wapya kwa ajili ya kuomba mkopo kutokana na mchakato huo kufungwa.

Alisema tofauti na tume ya vyuo vikuu ambayo inaweza kufungua udahili na kutoa majina ya wale waliopata nafasi ndani ya siku tatu, HESLB huhitaji muda mrefu kupitia taarifa za waombaji hadi kutoa matokeo.

Kuhusu marejesho ya mikopo kwa wahitimu wa elimu ya juu waliokopeshwa na bodi hiyo, Mwaisobwa alisema idadi kubwa ya wadaiwa na waajiri wamejitokeza kulipa madeni yao na kuhakiki taarifa za madeni yao.

“Idadi kubwa ya wadaiwa wamejitokeza kulipa na kuhakiki taarifa zao, pia hata waajiri wengi wamejitokeza na kuthibitisha hili ni kwamba mapato tuliyokusanya yameongezeka kwa kiasi kikubwa” alisema Mwaisobwa.

Alisema wanaokaidi kulipa, watambue kuna sheria zitakazowabana, ikiwa ni pamoja na vifungo na penati, lakini hilo halitangulizwi bali mpaka mkopaji aonekane kukaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles