Na Bright Masaki, Dar es Salaam
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeifungia Televisheni ya Wasafi Tv kutoa huduma kwa muda wa miezi sita kuanzia kesho January 6 mwaka huu hadi Juni 2021 kwa makosa ya kukiuka taratibu za utangazaji.
Adhabu hiyo imetolewa leo Dar es Salaam na Kaimu Mkurugezi wa Sheria (TCRA), Johannes Karungura.
Maamuzi hayo yanakuja kufuatia maudhui ya picha jongefu yaliyomwonesha msanii wa bongo Fleva, Gift Stanford maarufu kama Gigy Money akicheza utupu kinyume na kanuni za maadili katika tamasha la Tumewasha Live Concert lililorushwa Januari Mosi, 2021 kuanzia saa mbili hadi saa tano usiku.
Aidha, kituo hicho cha Wasafi Tv wanatakiwa kutumia siku ya leo kuomba radhi kwa watazamaji wake kufuatia ukiukaji huo na wakikaidi hatua zaidi za kisheria na udhibiti zitachukuliwa.