29.9 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

TCRA yafanya mabadiliko ya vifurushi vya simu

Na Brighiter Masaki, Dar es Salaam

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), baada ya uwepo wa malalamiko ya vifurushi kutoka kwa watumiaji wa simu, imepitisha mabadiliko ya kanuni ndogo za Vifurushi ikiwemo mteja kuhamisha uniti za kifurushi kwenda kwa mtu mwingine.

TCRA kama Mdhibiti wa sekta ya Mawasiliano ya Kieletroniki na Postal nchini, pamoja na mambo mengine, ina jukumu la kusimamia gharama na tozo katika huduma za Mawasiliano zinazotolewa na watoa huduma.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, leo Jumanne Machi 2, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba, amesema dhumuni la juhudi hizo ni kupunguza tofauti kubwa iliyokuwepo kati ya bei ya Vifurushi na bei za kutumia huduma bila kujiunga na Vifurushi.

Amesema katika kutekeleza majukumu yake TCRA imekuwa ikichukua hatua mbalimbali zinazolenga kuhakikisha mahitaji ya wadau wa pande zote (Serikali, Watoa huduma na Watumiaji wa huduma) uanafikiwa kupitia huduma husika.

Miongoni mwa Kanuni ndogo zilizobadilishwa ni kwamba mtoa huduma hatatoa huduma za Vifurushi bila kibali cha Mamlaka.

Mtoa huduma atatoa taarifa kila wakati matumizi ya kifurushi yatakapofikia asilimia 75 na 100 kwa Vifurushi vya muda wa maongezi Data na Ujumbe mfupi (SMS).

“Mtoa huduma ataweka utaratibu au mfumo wa kumwezesha mtumiaji wa huduma kuhamisha uniti za kifurushi kwenda kwa mtumiaji mwingine ndani ya mtandao wake kwa masharti ya kiasi cha chini kuhamisha kutakuwa 250mb.

“Mtoa huduma ataweka utaratibu wa kumwezesha aliyejiunga na kifurushi chochote kuendelea kutumia muda au uniti za kifurushi ambazo zitakuwa zimesalia ndani ya muda wa matumizi uliowekwa kwa kununua tena kifurushi hicho hicho kabla ya kumalizikakwa muda wake,” amesema Mhandisi Kilaba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles