27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Tchetche: Nimechoka kucheza Tanzania

Kipre Tchetche
Kipre Tchetche

Na SAADA SALIM -DAR ES SALAAM,

MSHAMBULIAJI wa timu ya Azam FC, Kipre Tchetche, amedhamiria kuachana rasmi na klabu hiyo kwa kuendelea kuushinikiza uongozi umruhusu kuondoka ili akatafute maisha sehemu nyingine.

Tchetche ambaye ni raia wa Ivory Coast, hadi sasa hajajiunga na wenzake katika mazoezi ya kujiandaa na michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao na Kombe la Shirikisho barani Afrika mwakani.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Tchetche alisema anasubiri ruhusa ya kuondoka Azam kwani amepata dili katika klabu moja kubwa nchini Misri.

Tchetche alisema amefanya mawasiliano ya barua pepe na viongozi wa klabu hiyo akiomba kuondoka lakini hajajibiwa chochote, huku akidai kuwa anahitaji baraka zao kabla ya kucheza timu nyingine.

Straika huyo ambaye ni kinara wa kupachika mabao Azam, alisema anahitaji kubadili maisha ya soka kwa kuwa amecheza Ligi Kuu ya Tanzania kwa muda mrefu hivyo amechoka.

“Juhudi zangu za kufanya mawasiliano na viongozi na pia wakala wangu kuwatumia ujumbe wa barua pepe ili kufikia makubaliano nikacheze Misri baada ya kupata ofa, zimegonga mwamba kwani hawajibu lolote.

“Nimebakiza mkataba wa mwaka mmoja, lakini  nimepata ofa nzuri Misri ila viongozi wangu wamekata mawasiliano na mimi, kwa sasa sina furaha ya kucheza soka nchini Tanzania,” alisema Tchetche.

Naye Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, alikiri kwamba ni kweli Tchetche hajaripoti mazoezini na pia hajatoa sababu za msingi za kuchelewa, hali inayowapa wasiwasi  kutokana na kulazimisha kutaka kuondoka.

Kawemba alisema kama amepata timu  nyingine inatakiwa kufuata taratibu za usajili  kwani thamani ya mchezaji huyo ni dola 150,000  za Marekani sawa na Sh milioni 322.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles