22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

‘TCB wasadieni Wanawake kutoka kwenye mikopo umiza’- Mtaka

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka, amesema kama Benki ya Biashara Tanzania (TCB) inataka kufanikiwa zaidi kibiashara hainabudi kujikita katika kuwasaidia Wanawake wajasiriamali kutoka kwenye mikopo umiza na kuweza kukopa katika benki hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka.

Akizungumza leo Jumatano Septemba 8, 2021 wakati wa uzinduzi wa kongamano la wanawake na biashara ambalo liliandaliwa Benki ya Biashara Tanzania (TCB) Mkuu huyo wa Mkoa amesema kama benki hiyo inataka kufanikiwa zaidi ni lazima ijikite kutoa mikopo kwa wanawake wajasiriamali ili waweze kujisaidia katika biashara zao.

Katika kongamano hilo wanawake wajasiriamali walipata fursa ya kuifahamu TCB ambapo pia ziliwasilishwa mada mbalimbali ikiwemo nafasi ya mwanamke katika kukuza uchumi wa Taifa,ambapo jumla ya washiriki 350 hasa wanawake walishiriki.

Amesema changamoto kubwa kwa wanawake ni kukopa mikopo umiza lengo likiwa ni kufanikisha ndoto zao ambapo amedai jambo hilo limekuwa likiwarudisha nyuma hivyo Benki hiyo inatakiwa iwasaidie wapate mikopo yenye riba nafuu.

“Mkurugenzi (Sabasaba Moshingi) tafuta ‘position’ ukijikita kwa wanawake benki yako itakuwa kubwa,hawa wanawake unaowaona hapa wanakopa Sh 500,000 marejesho Sh milioni 2 au nakosea (wanashangilia) wasaidieni hawa wajasiriamali kutoka kwenye mikopo umiza,” amesema Mtaka.

Vilevile,Mtaka ameitaka TCB kuzifuata fursa ambazo zipo katika maeneo mbalimbali na kisha kutoa fedha kwa wanawake ili waweze kujikwamua kiuchumi kwa kufanya biashara katika maeneo mbalimbali.

“Hapa nitawaleta watu wanaojenga Standard Gauge,Tarura na wale wa Bomba la Mafuta waje waseme fursa kwao zipo katika maeneo yapi halafu nyinyi muwape fedha wanawake ili ikiwezekana wasambaze vyakula katika miradi hii,” amesema.

Pia, amesema jukwaa la wanawake na biashara linaendana na mpango wa Rais Samia Suluhu Hassan wa kuongeza ushiriki wa wanawake katika kushiriki na kusimamia uchumi wa Taifa.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa TCB,Sabasaba Moshingi amesema atashirikiana na Mkuu wa Mkoa kuhakikisha wazifuata fursa hizo ikiwemo kwenda katika baadhi ya Mikoa.

Hata hivyo, amesema benki hiyo inawajibu kuupa kipaumbele uwekezaji wa wanawake na maendeleo yao baada ya Serikali kuziunganisha shughuli zake na zile za iliyokuwa Benki ya wanawake Tanzania.

Amesema lengo la kongamano hilo ni kuwakusanya wanawake ili waweze kujadiliana kwa pamoja jinsi ya kukuza biashara zao na kuweza kufanikiwa katika maisha yao hivyo kuikwamua jamii kiuchumi.

Aidha,amesema kwa sasa zipo huduma maalum zinazowalenga kina mama kama akaunti ya Tabasamu na dirisha maalum kwa ajili yao kwenye matawi  ya benki na huduma za bima maisha kwa vikundi ambavyo wanachama wake wengi ni wanawake.

Naye,Mbunge wa Viti Maalum,Fatma Toufiq amewataka wanawake nchini kupendana kuheshimiana pamoja na kuchangamkia fursa mbalimbali ambazo zimekuwa zikijitokeza huku akiiomba Serikali kuendelea kuwapa kipaumbele katika mambo mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles