22.5 C
Dar es Salaam
Saturday, June 3, 2023

Contact us: [email protected]

TBL Plc yawezesha wakulima 450 wa mtama kuhudhuria maonyesho ya TARI

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Kampuni ya Tanzanian Breweries Public Limited Company (TBL Plc) imefadhili wakulima 450  wa mtama inaoshirikiana nao kutoka wilaya za  Kongwa,Mpwapwa,Chamwino mkoani Dodoma kushiriki maonyesho ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) yaliyofanyika mwishoni mwa wiki.

Meneja kilimo wa Tanzania Breweries Limited (TBL), Joel Msechu (Kulia) akiongea na wakulima wa mtama wanaoshirikiana na kampuni hiyo wakati walipotembele shamba la mtama la mfano wakati wa maonyesho ya TARI yaliyofanyika Hombulu mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki wakulima wa mtama katika shamba la mfano wa TARI wakati wa maonyesho hayo.

Wakulima wadogo ni wadau muhimu wa kampuni ya TBL kwa kuiuzia malighafi, kampuni inanunua asilimia 74 ya malighafi kutoka nchini ikiwemo tani 9,000 za mtama kwa ajili ya kutengeneza chapa maarufu za vinywaji vya bia aina ya Eagle na Bingwa.

Mwaka jana TBL Plc kwa kushirikiana na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Shirika la Farm to Market Alliance (FtMA) kuendesha mradi wa majaribio kwa kuwawezesha wakulima 2,000 mkoani Dodoma kwa kuwapatia mbegu bora, huduma ya bima ya kilimo, itifaki za usimamizi wa mazao, ushauri wa kilimo kwa ajili ya kuhakikisha wanaongeza mavuno na soko la uhakika wa mavuno yao.

Kampuni hiyo pia ilishirikiana na TARI kufanya utafiti na kukuza mbegu za mtama ambazo zinafaa zaidi kwa ardhi na mazingira ya hali ya hewa ya Tanzania.

Mradi huo wa majaribio ulipata mafanikio makubwa, ulifanikisha ongezeko la uzalishaji wa zao la mtama kwa asilimia 70. TBL Plc sasa imeendeleza mradi huo kwa kufanya kazi na wakulima 4,000 katika msimu huu wa 2021 ambapo imewapatia tani 22 za mbegu za mtama kutoka katika makampuni ya Namburi ya Mbeya na TARI tawi la Dodoma.

Maonyesho haya ya TARI yanawakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo kwa kuonyesha ushirikiano wao katika kuendeleza sekta hiyo nchini sambamba na kufanyia kazi changamoto wanazokutana nazo wakulima katika kazi yao.

Wakulima waliopata ufadhili wa TBL Plc wameweza kujifunza mbinu mbalimbali za kuendesha kulimo cha kisasa na matumizi ya teknolojia za kisasa zitakazowawezesha kuongeza uzalishaji zaidi pia wameweza kukutana na wadau muhimu katika sekta hiyo.

Akiongea kwa niaba ya wakulima wa mtama walioshiriki, Leonard Yeramu, kutoka Kongwa aliishukuru TBL kwa kuwawezesha kushiriki kwa kuwa wamejifunza mbinu mbalimbali kuhusiana na kilimo cha mtama

Kwa kusaidia wakulima  moja kwa moja kupata  ujuzi, kushikamana na kuwawezeshwa kifedha, TBL inawasaidia kuongeza  uzalishaji wao,kupata faida zaidi, na utumiaji mzuri wa maliasili.

Mipango hii  inaenda sambamba  na  malengo  ya kampuni mama ya TBL ya ABInBEV kwa asilimia 100% ya kuwapatia wakulima wadogo ujuzi,kuwaunganisha pamoja, na kuwawezesha kifedha hadi ifikapo mwaka 2025.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,270FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles