TBL kushiriki siku 16 kupinga ukatili wa kijinsia

0
889

Mwandishi Wetu-Dar es Salaam

KAMPUNI ya Tanzania Breweries Limited (TBL) kwa imesema inaungana na mashirika yanayopinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutetea haki za binadamu katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi- Kitengo cha Dawati la Jinsia  kituo cha Chang’ombe,Dar es Salaam na Kisarawe mkoani Pwani.

Maadhimisho haya  huandaliwa kila mwaka na Shirika lisilo la kiserikali la WiLDAF kwa kushirikiana na mtandao wa mashirika yanayopinga ukatili wa kijinsia nchini (MKUKI), wadau wa maendeleo na taasisi mbalimbali za kiserikali na za binafsi.

Mwaka huu, maadhimisho haya yamelenga  zaidi kupinga vitendo vya ubakaji na kuelimisha jamii ya Watanzania juu ya athari za ukatili wa kingono na kusisitiza jukumu la kila mmoja wetu kubadili fikra zetu, kuvunja ukimya na kuchukua hatua juu ya vitendo vya ukatili huo. 

Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo,Abigail Mutaboyerwa alisema Dar es Salaam jana, kuwa mwaka jana kampuni hiyo ilitumia maadhimisho hayo kwa kuendesha kampeni yake inayolenga kuleta mabadiliko kwenye jamii  iitwayo “#Isiwesababu”kuelimisha jamii kuhusu unywaji wa kiustaarabu na kutokutumia pombe kama sababu ya unanyanyasaji wa kijinsia.

Alisema mwaka huu,itatumia njia mbalimbali kutoa elimu ya uelewa kwa jamii, ikiwamo kuendesha semina kwa wafanyakazi wake na jamii maeneo mbalimbali kwa kushirikiana na jeshi la polisi kitengo cha dawati. 

Alisema kampeni  ya #IsiweSababu itaendelea kutoa elimu mbalimbali,ikiwamo kuhimiza jamii kuchukua hatua na kuvunja ukimya na pale pombe kutumiwa kama sababu moja wapo za vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Alisema mbali na kujua jukumu la kampuni kuelimisha jamii kuhusu unywaji wa kistaarabu,ina sera inayohamasisha unywaji wa pombe kwa kistaarabu ili kuepusha madhara mbalimbali ya unywaji wa pombe kupita kiasi ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia.

 Alisema anaamini ukatili wa kijinsia unaweza kutokomezwa endapo jamii nzima itashirikiana na kuahidi kuchukua hatua kukemea vitendo hivyo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here