20.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 28, 2022

TBL FC KUSHUHUDIA MECHI LIGI KUU YA UINGEREZA

Na GLORY MLAY-DAR ES SALAAM


BINGWA wa mashindano ya soka ya makampuni yaliyoandaliwa na Benki ya Standard Chartered, TBL FC, inatarajiwa kuondoka Septemba mwaka huu kuelekea nchini Uingereza, kutembelea klabu maarufu ya Liverpool pamoja na  kukutana na wachezaji mashuhuri wanaoichezea klabu hiyo.

Timu hiyo itakuwa nchini Uingereza kati ya Novemba 8 hadi 10, mwaka huu na itashuhudia mechi ya mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza, kati ya  timu ya Fullham na Liverpool utakaopigwa katika Uwanja wa Anfield.

Akizungumza Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group, Roberto Jarrin, aliipongeza Benki ya Standard Charted nchini kwa ubunifu mkubwa  wa kuwaunganisha wateja wake kupitia nyanja ya michezo sambamba na utoaji huduma bora kwa wateja wake.

Naye, nahodha wa timu hiyo, Lupa Mwanjopa, alieleza kuwa wamefurahi kupata fursa hiyo ya kwenda nchini Uingereza sambamba na kutembelea klabu ya Liverpool na kukutana na wachezaji nguli wa timu hiyo.

Mkuu wa Uhusiano na Masoko wa Benki hiyo, Juanita Mramba, alisema mbali na kutembelea klabu hiyo, pia watapata nafasi ya kufanya mazoezi katika Uwanja wa Anfield pamoja na kwenda kuangalia mchezo wa wapinzani wa Liverpool.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,097FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles