25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

TBA kukarabati majengo shule ya sekondari Juhudi Dar

Koku David – Dar es Salaam

Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), umeahidi kusaidia ujenzi na ukarabati wa majengo katika shule ya sekondari ya Juhudi iliyopo eneo la Mboto, Ilala jijini Dar es Salaam.

Shule hilo iliyoanzishwa na kuendelezwa na wananchi wa ene hilo, inakabiliwa na uchakavu wa miundombinu ya majengo ya ofisi na madarasa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana katika mahafali ya tatu ya kidato cha sita katika shule hiyo baada ya kusikiliza risala iliyosomwa na mkuu wa shule na ile ya viongozi wa serikali ya wanafunzi, Kaimu Mtendaji Mkuu wa TBA, Said Mndeme amesema watakarabati madarasa 10 ya wanafunzi ikiwa ni pamoja na ofisi kwaajili ya serikali ya wanafunzi ambao wanafanya Kazi bila ya kuwa na ofisi.

“Uchakavu wa miundombinu ya majengo ya ofisi na madarasa vinasababisha walimu na wanafuzi wa shule hii kusoma katika mazingira magumu huku walimu wakifanyakazi katika mazingira magumu hivyo tukiwa kama wadau wa sekta ya elimu upande wa miundombinu ya majengo na majenzi tutasaidia kukarabati majengo 10 ya madarsa, majengo ya utawala na ofisi za walimu.

“Shughuli za ukarabati huo zimeshaanza kwa hatua za awali na nimeambatana na wataalamu kutoka TBA, kabla ya kuanza kwa mahafali haya tulitembelea na kuanza kufanya tathmini ya majengo yanayohitaji ukarabati,” amesema Mndeme.

Ameongeza kuwa shule hiyo imekuwa ikiibua na kuendeleza vipaji vya wanafunzi katika sekta ya michezo lakini inakabiliwa na changamoto ya kukosa viwanja na miundombinu mingine ya michezo na kwamba katika kuhakikisha changamoto hiyo inatatuliwa watasaidia kutafuta wadau wa michezo ili walitafutie utatuzi.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,301FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles